Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Aswege Enock Kaminyoge siku ya tarehe 25/3/2025 amefanya kikao kazi na viongozi wa Halmashauri zote mbili pamoja na wa taasisi za serikali zilizopo katika Wilaya ya Bunda.
Mh.Kaminyoge alisema lengo kuu la kikao hiki ni kujitambulisha kwenu nikiwa ndiye Mkuu wa Wilaya hii baada ya mabadiliko yaliyofanywa na Mh. Rais siku chache zilizopita, na pia kuwatambua nyie viongozi wote mliopo mahali hapa, pamoja na kuomba ushirikiano wenu ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano katika kuhakikisha tunawaletea wananchi wa Wilaya hii maendeleo na kuhakikisha wanaishi kwa amani, furaha na usalama.
Katika kikao hicho viongozi kutoka ngazi ya vijiji, kata na mitaa wote walihudhuria, ambapo walimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwaalika katika kikao hicho na kumuahidi kumpa ushirikiano wote katika kuhakikisha wanawaletea maendeleo wananchi wa Bunda katika katika sekta zote za elimu, Afya, maji, nishati na miundombinu iliyobora na mizuri katika kuhakikisha wanaleta na kukuza maendeleo ya wanaBunda.
Mh. Kaminyoge aliweza kusikiliza kero na changamoto ambazo viongozi hao wamekuwa wakizipitia katika utendaji wao wa kazi, ambapo kupitia wakuu wa idara na vitengo waliweza kuzitatua na kuwafafanulia kulingana na Sheria kanuni na taratibu za kazi.
Mkuu wa Wilaya aliwaomba viongozi hao kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja na kuhakikisha Kila mtu anatimiza majukumu yake ya KAZI kwa kufuata kanuni, taratibu na Sheria za kazi, na pale wanapohitaji kuonana nae milango ya ofisi yake IPO wazi na Kila mtu anaruhusiwa kuja kuongea nae pale anapohitaji ufafanuzi au ushirikishwaji wake kama Mkuu wa Wilaya.
Aidha, Mh. Kaminyoge aliwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa idara na vitengo kuhakikisha wanaandaa miradi ambayo itatembelewa na mwenge wa uhuru, 2025 wakishirikiana na taasisi katika kuhakikisha maandalizi ya mapokezi ya mwenge yanaanza mapema kwa kubainisha miradi yote na njia
0 comments:
Post a Comment