Home » » MWENGE WA UHURU, 2024 WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALAMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

MWENGE WA UHURU, 2024 WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALAMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

Mwenge wa uhuru, 2024 umezindua miradi minne ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, siku ya tarehe 2/8/2024.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava amezindua mradi wa huduma za jamii, ambayo ni nyumba ya kulala wageni yenye thamani ya Tshs million 230 iliyopo Nyamuswa.

Pia, alizindua nyumba ya watumishi (3in1), iliyopo Kata ya Hunyari katika kituo cha Afya Hunyari na shule ya Sekondari ya Mariwanda, na mradi wa maji Sanzante.

Ndugu Mnzava alisisitiza wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuhakikisha wanashiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuhakikisha wanaenda kupiga kura ili waweze kuchangua viongozi Bora, na aliwasisistiza kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kuhakikisha kila kaya inapanda Miti mitano.

Mbio za Mwenge wa uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, imetembelea, kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo.

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa