MAMA MACHEL AISHAURI MARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mjane wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Graca Machel (katikati) akiwasili mjini Musoma kuanza ziara ya siku tatu mkoani Mara kuangalia maendeleo ya mradi wa kusaidia watoto ambao wako nje ya mfumo wa shule unaotekelezwa na Taasisi ya Graca Machel Trust (GMT) kwa ushirikiano wa Mara Alliance na Mkoa wa Mara. Wanaompokea ni Mwenyekiti wa Mara Alliance, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma, Michael Msonganzila (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi (kulia). (Picha na Mugini Jacob).
UONGOZI wa mkoa wa Mara umeshauriwa kuona umuhimu wa kuweka mpango shirikishi wa muda mrefu utakaosaidia watoto ambao wapo nje ya mfumo wa shule ndani ya mkoa huo, ili kupata elimu.
Ushauri huo ulitolewa na aliyekuwa mke wa rais wa Msumbiji, Samora Machel, Graca Machel. Graca pia alikuwa mke wa rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Mama Machel alitoa ushauri huo katika mkutano maalumu na wadau ambao ulitumika kutoa matokeo ya utafiti wa watoto ambao wapo nje ya mfumo wa shule.
Utafiti huo umebaini watoto 11,666 wenye umri kati ya miaka saba hadi 17 ambao wako nje ya mfumo ya shule chini ya mradi wa miaka miwili ambao unatekelezwa na taasisi ya Graca Machel Trust (GMT) kwa ushirikiano wa Mara Alliance na serikali ya mkoa wa Mara.
Aidha, baada ya utafiti huo watoto hao wataandikishwa kupata elimu chini ya Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (Memkwa). Mama Graca alisema lengo la mradi huo ni kusaidia watoto 20,000 ambao wapo ya nje ya mfumo wa shule kwa sababu mbalimbali.
“Tunahitaji mpango wa miaka mitano au 15 ili kuondoa hili tatizo na huu ni mwanzo wa safari kuondoa tatizo la watoto ambao wako nje ya mfumo wa shule”, alisisitiza Mama Graca.
Utafiti huo umefanywa katika halmashauri tano za wilaya za Tarime, Bunda, Butiama na Musoma.
Umeonesha kuwa Wilaya ya Bunda inaongoza kuwa na watoto wengi walio nje ya shule kwa asilimia 33, Tarime (31), Butiama (26) na Musoma (10).
Mkuu wa Kitengo cha utafiti na machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Uchumi na Jamii (ESRF) ambao wamefanya utafiti huo Dk Fortunata Makene, alisema utafiti huo ulifanyika nyumba kwa nyumba.
Dk Makene alisema ni muhimu kuwepo na mpango wa kukabiliana na tatizo la ndoa za utotoni katika mkoa huo wa Mara .
Kwa upande wake, mdau wa elimu mkoani humo, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma, Michael Msonganzila, alisema ni habari njema kuona kuwa GMT, Mara Alliance na Serikali wameungana kusaidia watoto ambao wako nje ya mfumo wa shule chini ya mpango wa Memkwa.
Akizungumza katika hafla hiyo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Vicent Naano alimhakikishia Graca kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kuwa tatizo la watoto walio nje ya mfumo wa shule linabaki kuwa historia na kufanya mradi huo kuwa na mafanikio makubwa.
Graca aliwasili mjini Musoma Machi 13 kwa ziara ya siku tatu mkoani Mara kuangalia maendeleo ya mradi wa kusadia watoto ambao wako nje ya mfumo wa shule unaotekelezwa na taasisi yake kwa ushirikiano wa Mara Alliance na Serikali ya Mkoa wa Mara.

CHANZO GAZETI LA HABARI LEO

MAZISHI YA MAREHEMU MTONGORI MANG'ACHE YAFANYIKA TARIME MKOANI MARA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime, Mchungaji Canon Yohana Chacha (katikati), akiongoza ibada ya mazishi ya Anna Mtongori Mang'ache hii leo katika Mtaa wa Kenyamanyori, halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara.

Wengine ni Mchungaji wa Kanisa la Angilikana Parishi ya Kenyamanyori Tarime, Wyclif Chereme (kulia) pamoja na Mchungaji wa Kanisa Anglikana Parishi ya Kemange Tarime, Charles Mwita (kushoto).

Marehemu Anna Mtongori Mang'ache aliyezaliwa mwaka 1931 Kenyamanyori Tarime, alifariki dunia alihamisi iliyopita Machi 02,2017 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza.

Familia ya Mang'ache inawashukuru Madaktari wote wakiwemo wa Hospitali ya Winani Tarime, CF na Bugando Jijini Mwanza, jeshi la polisi, viongozi wa dini, ndugu, jamaa na marafiki kwa ushirikiano wao wa dhati katika kumuuguza marehemu Anna Mtori Mang'ache na hata katika kufanikisha mazishi yake. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina!
#BMGHabari
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime, Mchungaji Canon Yohana Chacha (katikati), akiongoza ibada ya mazishi ya Anna Mtongori Mang'ache 
Mchungaji wa Kanisa la Angilikana Parishi ya Kenyamanyori Tarime, Wyclif Chereme, akizungumza kwenye ibada ya mazishi hayo
Mwinjilisti Foredy Qojedy, akisoma maandiko ya biblia kwenye mazishi hayo wakati wa ibada
George Binagi akisoma historia fupi ya marehemu kwa niaba ya wanafamilia wakati wa ibada ya mazishi hayo
Wanafamilia wakiwemo watoto wa marehemu Anna Mtongori Mang'che
Kaka wa marehemu, Mzee Maina Binagi, akitoa salamu za familia kwenye mazishi hayo
Wanafamilia wakiuaga mwili wa marehemu
Mwita Mang'ache na Makorere Mang'ache ambao ni miongoni mwa watoto wa marehemu wakiuaga mwili
Mmoja wa watoto wa marehemu, Koplo Thomas Binagi Mang'ache (kulia) na mkewe (katikati) na ndugu, jamaa na marafiki wakiuaga mwili wa marehemu
Kaka wa marehemu, Profesa Lloyd Binagi na waombolezaji wengine wakiuaga mwili wa marehemu
Kaka wa marehemu Mzee Chacha Binagi na waombolezaji wengine wakiuaga mwili wa marehemu
Kaka wa marehemu Mzee Maina Binagi na waombolezaji wengine wakiuaga mwili wa marehemu
Wajukuu za merehemu wakiuaga mwili wa marehemu
Ndugu, jamaa, marafiki pamoja na watoto wa marehemu, wakitoa salamu zao za mwili kwa mwili wa marehemu
Ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wajukuu wa marehemu, wakitoa salamu zao za mwili kwa mwili wa marehemu
Ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wajukuu wa marehemu, wakitoa salamu zao za mwili kwa mwili wa marehemu
Jeneza lenye mwili wa marehemu likipelekwa malaloni
Jeneza lenye mwili wa marehemu likishushwa malaloni
Ndugu, jamaa na marafiki wakirusha udongo malaloni ishara ya kuuaga mwili wa marehemu
Mtoto wa marehemu Mwita Mang'ache na mkewe wakiweka mashada
Mtoto wa marehemu Chacha Mang'ache na mkewe wakiweka shada malaloni
Mtoto wa marehemu na mkwelima wa marehemu wakiweka mashada
Kaka wa marehemu Mzee Maina Binagi na wake zake, wakiweka mashada
Mjukuu wa marehemu akiweka shada
Mtoto wa Marehemu Koplo Thomas Binagi Mang'ache akiwaongoza wajukuu wa marehemu wakiweka mashada
Wajukuu wa marehemu wakiweka mashada
Diwani wa Kata ya Nkende, Daniel Komote, akiweka shada kwa niaba ya viongozi wengine wa siasa
Wanafamilia wakiweka mashada
Familia ya Mang'ache inawashukuru Madaktari wote wakiwemo wa Hospitali ya Winani Tarime, CF na Bugando Jijini Mwanza, jeshi la polisi, viongozi wa dini, ndugu, jamaa na marafiki kwa ushirikiano wao wa dhati katika kumuuguza marehemu Anna Mtori Mang'ache na hata katika kufanikisha mazishi yake. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina!

RAIS DKT. MAGUFULI AMSAIDIA DADA NEEMA MWITA WAMBURA ALIYEMWAGIWA UJI WA MOTO NA MUMEWE MKOANI MARA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Dada Neema Mwita Wambura (32) akizungunza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu akimshukuru kwa msaada aliompatia wa kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia Rais Dkt. Magufuli ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo pamoja na watoto wake watatu ambao kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpatia msaada Dada huyo kiasi cha Shilingi laki tano.  Dada Neema Mwita Wambura aliungua vibaya mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa unachemka jikoni na mume wake katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara.
 Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) ambaye amempa hifadhi Neema Mwita Wambura nyumbani kwake Tandika Davis Corner akiomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu kumshukuru mara baada ya kuzungumza naye kuhusiana na kumsaidia Dada Neema Mwita Wambura (32). Rais Dkt. Magufuli amempongeza Mama huyo Mjane ambaye ameonesha moyo wa kizalendo na kumpa hifadhi Dada huyo aliyemwagiwa uji wa moto na mumewe katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpa Mjane huyo kiasi cha Shilingi laki tano.
  Dada Neema Mwita Wambura (32) wakwanza kulia akiwa pamoja na Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) wakiwa ndani ya gari mara baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumsaidaia ili aweze kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
 Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimpokea Dada Neema Mwita Wambura (32) na kuanza mara moja kumfanyia tena uchunguzi wa afya yake katika majeraha aliyoyapata mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa ukichemka jikoni  kitendo kilichofanywa na mume wake.
 Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru akimjulia hali Dada Neema Mwita Wambura (32) mara baada ya kufikishwa tena hospitalini hapo. Dada Neema Mwita alifanyiwa upasuaji mara nne katika siku za nyuma hospitalini hapo Muhimbili ili kutibu majeraha yake hayo ya moto.
 Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura na Ajali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga akizungumza kuhusu hali ya mgonjwa Dada Neema Mwita Wambura (32) aliyefikishwa tena katika Hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi wa Afya yake.
 Dada Neema Mwita Wambura (32) akiwa katika hali ya majonzi kufatia majeraha makubwa mwilini mwake kufatia kumwagiwa uji wa moto na mume wake mkoani Mara.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa ngozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  Dkt. Ibrahim Mkoma akizungumzia historia ya mgonjwa huyo ambaye yeye pamoja na jopo la madaktari bingwa walimfanyia upasuaji ili kutibu majeraha yake ya ngozi katika kipindi cha nyuma. PICHA NA IKULU

WACHIMBAJI WADOGO KUMILIKISHWA ENEO LA STAMICO, BUHEMBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Mmoja wa wachimbaji waliokolewa katika ajali ya kifusi akimweleza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) jinsi ajali hiyo ya kufikiwa na kifusi wachimbaji 18 ilivyotokea. Katikakti  anayesikiliza ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje.
 Mmoja wa wachimbaji wadogo akishuka chini ya shimo la kuingilia katika mgodi kwa ajili ya kusaidia shughuli za uokoaji kufuatia ajali ya kufukiwa na kifusi wachimbaji 18 katika eneo la Buhemba mkoani Mara.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa  North Mara (ACACIA)  ambao walishiriki katika zoezi la uokoaji wa wachimbaji wadogo kwa kutoa msaada wa mashine ya kuvuta maji  na tope ili kuwezesha zoezi la ufukuaji kuendelea
 Sehemu ya Wachimbaji wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa ziara yake katika mgodi wa Buhemba  unaomilikiwa na STAMICO.
 Mmoja wa wachimbaji wadogo anayeshiriki zoezi la uokoaji katika eneo la Buhemba akimweleza Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo na wananchi waliokuwa eneo hilo kuhusu hali ilivyo ndani ya mgodi huo. 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiongea na wachimbaji wadogo katika eneo la Buhemba ambapo ajali ya wachimbaji wadogo walifukiwa na kifusi tarehe 13 Februari,2017.

Serikali imesema itatoa eneo linalomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Buhemba, Mkoani Mara kwa wachimbaji Wadogo wa Madini baada ya kufanyika kwa tathmini  na taratibu za kumilikishwa eneo ili wachimbaji hao wafanye shughuli hizo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu ikiwemo kulipa kodi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo leo tarehe 18 Februari,2017, wakati wa ziara yake katika mgodi huo ili kuangalia shughuli za uokoaji zinazoendelea katika mgodi huo, kufuatia  ajali ya kufukiwa na kifusi kwa Wachimbaji 18  iliyotokea tarehe 13 Februari,2017, ambapo wachimbaji 13 waliokolewa siku hiyo hiyo

Prof. Muhongo  amesema kuwa, wachimbaji hao hawakuwa na leseni wala vibali halali vilivyotolewa kwao  kufanya shughuli za utafutaji dhahabu na kwamba eneo hilo linamilikiwa kisheria na STAMICO kwa leseni  PL N0. 7132/2011, na kuongeza kuwa, wachimbaji hao walivamia eneo hilo ambapo ni kosa kisheria na wanatambulika kama wavamizi.

Ameongeza kuwa, shughuli za uchimbaji katika eneo hilo zilifungwa tangu mwaka 1971 ambapo awali eneo hilo lilikuwa chini ya wakoloni kabla ya kuwa chini ya uangalizi wa Jeshi  la Kujenga Taifa (JKT), Kampuni ya Meremeta na baadaye kuwa chini ya umiliki wa STAMICO.

Aidha, amezuia shughuli zote za uchimbaji kufanyika katika eneo hilo na kusema kinachofanyika sasa ni kuutafuta mwili wa mchimbaji mmoja ambaye bado haujatolewa. ''Hadi sasa wachimbaji 15 wamekwisha okolewa, bahati mbaya wawili walitolewa wamefariki na sasa tuendelee na zoezi la kutafuta mwili uliobaki,"ameongeza Prof. Muhongo.

Pia Prof Muhongo amewshauri wachimbaji hao kujiunga katika vikundi na kusajili vikundi hivyo ili kuwezesha shughuli zao kufanyika kwa kuzingatia taratibu za uchimbaji. "Jiungeni katika vikundi , lakini ni marufuku kwa familia moja kuwa na kikundi,"amesisitiza Prof. Muhongo


Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Viktori Mashariki Mhandisi Juma Sementa amesema kuwa, tayari Kanda hiyo imeshatoa maeneo yapatayo 35 kwa wachimbaji wadogo katika eneo la Lwabasi, mkoani humo na kueleza kuwa, leseni zote katika eneo hilo zinamilikiwa na wachimbaji  wadogo na hivyo kuwataka kufanya shughuli za uchimbaji kwa kuzingatia usalama na ikiwemo kulipa kodi.

Wachimbaji wengine wafukiwa na kifusi Mara

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Takriban mwezi mmoja tangu wachimbaji 15 wafukiwe na kifusi Nyarugusu wilayani Geita, balaa jingine la aina hiyo limetokea wilayani Butiama mkoani Mara.

Katika tukio la Butiama, watu 11 wameokolewa shimoni wakichimba dhahabu na kwa sasa wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Butiama kwa matibabu.
Mkasa huo umetokea katika Mgodi wa Buhemba na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi amesema kazi ya uokoaji inaendelea kwa ajili ya kuwatafuta watu wengine ambao ndugu zao hawajawaona na wanahisi walikuwamo ndani ya shimo hilo.
Amesema mmomonyoko wa udongo ndiyo uliosababisha kuporomoka kwa mashimo hayo ya muda mrefu licha ya kuwapo jua kali.
Aidha Nyamubi amesema mashimo hayo yaliyoachwa na mkoloni yako chini ya mwekezaji StanCom ambaye ndiye aliyekuwa akichimba dhahabu katika eneo hilo. Kufuatia tukio hilo, viongozi mbalimbali walifika kushuhudia uokoaji akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Charles Mlingwa.

Chanzo: Mwananchi

MKURUGENZI WA BUNDA AMVUA MADARAKA MWALIMU MKUU WA BUNDA B UDAGANYIFU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 

MAKALA:"KUENDELEZA MILA ZA UKEKETAJI NI KINYUME CHA HAKI ZA MTOTO"-SIHABA NKINGA

Katibu Mkuu Sihaba Nkinga akutana na Wazee wa Koo tano Mkoani Mara.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Wazee wa Kimila kutoka Koo Tano Mkoani Mara wamemuomba Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kuwawezesha kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.
Akiongea wakati walipokutana na Katibu Mkuu aliyepo Wilayani Tarime Mzee wa Koo ya Bukenye Mzee Elias Maganya alisema kuwa walishapata elimu kutoka kwenye Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) na changamoto ni jinsi ya kuzifikia koo nyingine Mkoani huko ili kuwezesha kuondoa kabisa mila hiyo.
“Tumechoka vitendo vya ukatili kwa watoto na vitendo visivyoturishisha sisi kama wazee, tutafanya kila jitihada kuweza kuondokana na vitendo hivi, tunahitaji ushiriki zaidi wa serikali na asasi nyingine zishirikiane na CDF ili kwa pamoja tuweze kufikia lengo tuliloliweka” Alisema Mzee Elias
Akitolea ufafanuzi suala hilo Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga amesema kweli upo umuhimu wa kutekeleza suala hilo la kupeleka elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili kuweza kuwasaidia watoto wakike.
Naye Mzee wa Kimila kutoka Koo ya Bukira Mzee Sinda Nyangore ameishauri serikali na mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka na kuacha utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo mbalimbali.
Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Sihaba Nkinga alitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Dawati la Jinsia katika wilaya hiyo na kujionea namna wanavyofanya kazi na jinsi wanavyokabiliana na changamoto mablimbali.
Aidha Bi. Sihaba aliwatembelea watoto wa kike waliopo katika mpango wa uendelezwaji kijasiriamali unaotekelezwa na Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) katika kata ya Manga Wilayani Tarime Mkoani Mara.
 
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa