Home »
» TANAPA yatoa ufananuzi kuhusu fidia kwa wananchi
TANAPA yatoa ufananuzi kuhusu fidia kwa wananchi
Shirika
la Hifadhi la Taifa (TANAPA) limesema ni jukumu la serikali kupitia
Wizara ya Maliasili na Utalii kuwalipa wananchi fidia za madhara
yanayosababishwa na wanyama pori ili kuiondolea TANAPA lawama.
Kauli
hiyo imetolewa hivi karibuni na Mhifadhi Mkuu ambaye ni Mkuu wa Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), William Mwakilema, wakati akijibu
maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua kwa nini TANAPA haiwalipi
wananchi fidia.
"TANAPA ni Shirika linalolipa kodi na mapato
mengine serikalini, hivyo serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii
ndiyo inalipa fidia hizo," alisema Mwakilema.
"Halmashauri za
wilaya wilaya zinafanya tathmini ya uharibifu na mkurugenzi wa wilaya
hutuna maombi hayo wizarani ambayo ina jukumu la kupeleka fedha za fidia
kwenye halmashauri," alisisitiza Mwakilema.
Alisema wananchi
wawabane wakurugenzi wa halamshauri kuwalipa fidia na si TANAPA.
Kutokana na hali hiyo baadhi ya viongozi wa vijiji, watendaji na
madiwani wa kata tatu za Nyanungu, Gorona na Nyarukoba wilayani Tarime
mkoani Mara wameitupia lawama halmashauri za wilaya.
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment