Serikali
imetakiwa kuingilia kati jengo lililojengwa kwenye zahanati ya kijiji
cha Kerende Kata ya Kemambo Wilayani Tarime kwa msaada wa Benk ya
maendeleo Afrika (African Development Bank)
Jengo
hilo ambalo limejengwa kwa ajili ya huduma ya akina mama na watoto
ambapo hadi sasa halijakabidhiwa na kusababisha popo kuendelea kuishi
na kushamili ndani ya jengo baada ya jengo hilo kukaaa mda mrefu bila
kutumika.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kerende Mambaga Mohamed kuwa Zahanati ya
Kerende haina jengo la huduma ya wajawazito huduma uipata nje ya jengo
la Zahanati kutokana na uhaba wa vumba vya kutolea huduma ya afya hivyo
anaitaka Serikali kuwafatilia wafadhili ili kukamilisha jengo.
Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya ya Tarime Charle samson amesema kuwa
ofisi yake haifahamu gharama zilizotumika katika ujenzi kwakuwa
wafadhili hawakuishirikisha idara ya afya nakwamba jengo hilo limejengwa
chini ya viwango vinavyotakiwa.
0 comments:
Post a Comment