Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mhe. Patrick W. Gumbo
Meya wa Manispaa ya Musoma |
Tangu kuasisiwa kwake Halmashauri ya Manispaa ya
Musoma imekuwa katika jitihada za makusudi katika kuwaletea wananchi
wake maendeleo katika nyanja zote ikiwamo uchumi, kijamii, kitamaduni,
kisiasa na uboreshaji miundombinu unaoendana na mabadiliko ya haraka
katika jamii. Kwa kawaida mchakato wa maendeleo ni endelevu, hivyo
Halmashauri ya manispaa ya Musoma imekuwa ikitumia rasilimali zake zote
kuhakikisha azma hii inatimilika.
Katika kipindi chote hiki Halimashauri imeshuhudia
mageuzi makubwa ya kiutendaji kitaifa na kimataifa. Hali hii inatoa
tafsiri pana kuwa nyakati zimebadilika sana. Katika dhana hii serikali
imekuwa ikitekeleza programu mbalimbali ili kuendana na wakati na
mabadiliko ya mfumo wa kiutendaji yanayotokea duniani kote.
Serikali imekuwa katika utekelezaji wa programu ya
maboresho katikati ya Miaka ya 90 pamoja na programu nyingine nyingi
zilizofuata ili kuongeza ufanisi na tija katika kuwaletea wananchi
maendeleo. Aidha, mwaka 2011 serikali ilisaini mkataba wa kimataifa wa
makuballiano ya kuongeza uwazi serikalini (Open Government Partnership)
Mkataba uliolenga kuongeza ushirikishaji wa wananchi katika maendeleo
yao.
Ukamilishaji wa tovuti hii ni moja ya nyenzo muhimu
katika kuongeza ushirikishaji wa wananchi na kuongeza uelewa wao katika
masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Halmashauri yao. Imani yangu ni
kuwa wananchi wataitumia fursa hii muhimu kwa ajili ya maendeleo yao kwa
kupata taarifa mbalimbali ambazo zitawasaidia kuboresha shughuli zao
mbalimbali.
Tunaomba ushirikiano wenu katika katika utoaji wa
maoni juu ya namna bora ya kuboresha huduma zetu pamoja na kupata
taarifa zinazowahusu. Natoa wito kwa viongozi mbalimbali na watumishi
kuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa muhimu kupitia tovuti hii.
Mwisho tunatarajia kupata ushirikiano mzuri kwa wadau
wote katika upashanaji wa taarifa mbalimbali ambao unalenga kuleta
mafanikio katika manispaa yetu ya Musoma.
Ahsanteni
CHANZO TOVUTI YA MKOA WA MARA
0 comments:
Post a Comment