Home » » DC awaweka maabusu viongozi

DC awaweka maabusu viongozi


na Ahmed Makongo, Bunda
MAOFISA watendaji wawili wa kijiji na kata, pamoja na mwenyekiti wa kijiji, wanashikiliwa na Polisi wilayani Bunda, kutokana na kudharau agizo la mkuu wa wilaya hiyo la kushindwa kuwaalika wananchi kwenye mkutano wa hadhara.
Wanaoshikiliwa katika kituo kidogo cha Kibara, ni Boniface Manyonyi (45), ambaye ni kaimu ofisa mtendaji wa Kata ya Namuhura, Joseph Mfungo (60) ambaye ni kaimu ofisa mtendaji wa Kijiji cha Namuhura na Mwinamila Kalyaya (46) ambaye ni mwenyekiti wa kijiji hicho.
Viongozi hao walikamatwa jana kufuatia agizo la mkuu huyo mpya Joshua Mirumbe, baada ya kufika katika eneo la mkutano na kukuta wananchi wasiozidi 15, huku kukiwa hakuna hata mwenyekiti mmoja wa kitongoji.
Mirumbe alisema kuwa kitendo cha kutokuwepo kwa wenyeviti wa vitongojia katika mkutano huo ni dalili tosha kwamba viongozi hao hawakuwaalika wananchi licha ya kuagizwa kufanya hivyo.
Alisema kuwa huo ni uzembe mkubwa kwa viongozi hao kushindwa kuwaalika wananchi na kwamba ndiyo maana aliamuru polisi wawakamate na kuwasweka maabusu.
Mkuu huyo aliongeza kuwa alifanya hivyo kwa viongozi hao ili kuwakumbusha kuwa makini katika kutimiza wajibu wao.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa