Home » » PINDA AWASILI MUSOMA KWA MAZISHI YA MWALIMU WA MWALIMU NYERERE

PINDA AWASILI MUSOMA KWA MAZISHI YA MWALIMU WA MWALIMU NYERERE



Shomari Binda, Musoma- Mara yetu Blog
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewasili Mjini Musoma mchana huu kwa ajili ya kuongoza viongozi wa Serikali katika kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Mwalimu wa Mwalimu Nyerere Mzee James Irenge aliyefariki dunia nyumbani kwake  maeneo ya Mwisenge katika Manispaa ya Musoma.

Katika uwanja wa ndege Mjini Musoma Waziri Pinda amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Stevin Wasira, Mbuge wa Jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Wananchi.
 
Mzee Irenge amefariki akiwa na umri wa miaka zaidi ya 120, na kwamba alimfundisha Mwalimu Nyerere katika Shule ya Mwisenge, kati ya mwaka 1934-1936.

Licha ya umri wake mkubwa, bado alikuwa na uwezo wa kusoma na kuandika mwenyewe bila kutumia miwani wala kusaidiwa.

Wiki kadhaa zilizopita, aliandika barua yake ya mwisho kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimshuru kwa kumwezesha kumlipia fedha za dawa na chakula mambo yaliyokuwa kilio chake cha siku nyingi.

Mwalimu James Irenge atazikwa jioni ya leo katika kijiji cha Busegwe kilichopo katika Wilaya ya Butiama Mkoani Mara.
 
Blogzamikoa
www.blogszamikoa.blogspot.com

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa