Augustine Mgendi
BUHEMBA
WANANCHI vijiji Vitatu wanaozungukwa na Mgodi wa
Buhemba wilaya ya Butiama mkoani Mara wamesema
kuwa wanakusudia kuishitaki Serikali ya Tanzania katika Taasisi za Umoja wa
Mataifa zinazohusika na haki za binadamu
ikiwa ni shinikizo la kulipwa fidia ya shilingi Bilioni 30.
Mbali na kusudio hilo la kuelekea umoja wa Mataifa
lakini pia wananchi hao wamesema kuwa wanakusudia kumuona Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kumueleza madhara yaliyosababishwa na Mgodi
huo ambao ulidaiwa kumilikiwa na Serikali kupitia Kampuni ya Meremeta.
Wananchi hao kutoka vijiji vya
Tarani,Biatika na Magunga huku wakiomba Wabunge kuungana na kutoipitisha Bajeti
ya Wizara ya Nishati na Madini had hapo Serikali itakapo wafidia.
Akiongea
na waandishi habari katika eneo hilo la Buhemba,Diwani wa kata ya Buhemba
Boniphace Masero amesema kuwa Mgodi huo umeachia athari kubwa kutokana na
machimbo yaliyoachwa kuleta athari kubwa huku Ardhi yao ikiwa haina rutuba kutokana
na Kemikali zilizomwagwa katika eneo hilo
Amesema athari zingine zilizoletwa na Mgodi huo ni
pamoja na Shule iliyokuwa katika eneo hilo kubomolewa lakini walishindwa
kuijenga kama walivyokuwa wameahidi wahuska hao wa mgodi huku miundombinu ya
barabara nao ikiwa haifai kutumika.
“Huu Mgodi umetuachia madhara makubwa sana maana
Mashimo hayakufukiwa,Milima inaleta uchafuzi wa Mazingira,shule iliyokuwa
imejengwa hapa ilibomolewa,Nyumba zikabomoka kutokana na Baruti za mgodi,katika
hili sisi tunakusudia kumuona Rais ili tumueleze haya Manyanyaso tunayoyapata”
alisema diwani huyo
Diwani Masero ameongeza kuwa athari nyingine ni
pamoja na baadhi nyumba za wakazi wa eneo hilo kubomoka kutokana na baruti
zilizokuwa zikipigwa katika Mgodi huo lakini mpaka sasa hawajalipwa fidia na
hivyo wanawaomba Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kutoipitisha Bajeti ya wizara ya Nishati na Madini mpaka walipwe fidia yao
Aidha Pasta wa Kanisa la Anglikana Samweli
Nyakarungu alisema kuwa mgodi huo wa Buhemba ulikuwa ni Mgodi wa kitapeli
ambapo wahusika hao wamechuma raslimali za Taifa na kushindwa kufanya shughuli
za Maendeleo katika Jamii.
Pasta Nyakarungu alisema kuwa mbali na wawekezaji
hao wa Kitapeli kuiba mali ya Watanzania lakini pia wamesababisha madhara
makubwa kwa jamii ya Buhemba kwa kushindwa kujenga miundombinu ya barabara,kujenga
shule kama inavyotakiwa.
Kutoka na adha hiyo Pasta huyo alisema kuwa Serikali
imeshindwa kuwajali wananchi wake na hivyo wanawaomba Wabunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano kutoipitisha Wizara ya nishati na Madini mpaka hapo
wananchi wa eneo hilo watakapopata fidia yao.
“Hawa wawekezaji
mimi naona hawakuja hapa kwa lengo la kumsaidia mtu wa Buhemba huu Mgodi naona
ulikuwa wa Kitapeli kabisa,wamechuma raslimali za Taifa na kushindwa kumsaidia
mtu anayezungukwa na mgodi na hata kurekebisha miundombinu huska na hii
inaonyesha jinsi Serikali isivyojali wananchi wake” alisema Pasta Nyakarungu
Naye Mwalimu mstaafu Sita Nyamhanga na bi Hadja
Yasini walisema kuwa mgodi huo umewaachia matatizo makubwa ikilinganishwa
walivyokuwa wameahidiwa wakati wanaanza uchimbaji katika mgodi huo.
“Tunavyojua
ni kwamba wawekezaji wanapowekeza eneo lolote lazima watu wanaozungukwa na
Mgodi ule wanufaike lakini hapa Buhemba sisi wananchi ndiyo tumepat tabu kabisa
kwani mpaka sasa hatuna shule,barabara inayopitika muda wote,eneo letu limebaki
Jangwa huku wakina mama wanapata tabu kutafuta maji kutokana na vyanzo vingi
vya maji kuchafuliwa na mgodi” alisema Mwalimu mstaafu huyo.
Kwa upande wake Bi Hadja Yasini alisema kuwa
wanapata tabu hata kutafuta kuni kutokana na eneo kubwa la Buhemba kubaki
Jangwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kulingana na adha hiyo Bi Hadja alisema kuwa ni
vyema Waziri mwenye dhama huska akawasaidia watu wa Buhemba ili waweze kupata
fidia zao kutokana na madhara waliyoyapata kutokana na mgodi huo.
Mgodi wa Buhemba ambao ulianza kuchimbwa mwaka 2002
ni moja ya mgodi ambao ulikuwa ni mkubwa hapa nchini ukielezwa kumilikiwa na
Serikali na kufungwa mwaka 2006 huku ukiacha eneo hilo la Buhemba kupoteza
rutuba yake
ni moja ya mgodi ambao ulikuwa ni mkubwa hapa nchini ukielezwa kumilikiwa na
Serikali na kufungwa mwaka 2006 huku ukiacha eneo hilo la Buhemba kupoteza
rutuba yake
0 comments:
Post a Comment