ZAIDI ya watu 15 wakiwemo waandishi
wa habari, leo wamenusurika kifo,
baada ya magari matatu yaliyokuwa
kwenye msafara wa mwenge wa uhuru
kugongana katika kijiji
cha Kasahunga, kwenye barabara kuu ya
Bunda-Ukerewe,
wakati msafara wa mwenge huo ukielekea
kwenye mkesha
katika kijiji cha Kibara wilayani Bunda,
mkoani Mara.
Katika tukio hilo magari mawili yameharibika
vibaya, likiwemo la taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa
(Takukuru) walilokuwa wamepanda pia
waandishi wa vyombo
mbalimbali vya habari.
Watu walisema walishuhudia gari mali ya
halmasauri ya wilaya
lenye namba za usajili SM 8809,
likigonga kwa nyuma
gari ya TAKUKURU yenye namba za
usajili T. 645 BCT.
Hali hiyo ilisababisha magari mengine
kugongana
na mengine kuaacha njia likiwemo la TRA
lenye namba za
usajili STJ 9663, ambapo pia kama
zisingekuwa juhudi za
madereva wa magari mengine kufanya
jitihada za
makusudi kwa kuacha barabara na kuingia
upande mwingine
uhenda ingekuwa ajali kubwa sana.
0 comments:
Post a Comment