Mwandishi wetu, Mara
Yetu
SERIKALI wilayani
Bunda, mkoani Mara imewataka wakulima wote wa zao la pamba waliokopa pembejeo
kwa makampuni ya yanayonunua zao hilo, katika msimu wa kilimo uliopita
ifikapo septemba 30 mwaka huu wawe wamelipa madeni yao vinginevyo hatua kali za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mkuu wa wilaya ya
Bunda, Bw. Joshua Mirumbe, ametoa agizo hilo leo mjini Bunda, kwenye warsha ya
kuboresha kilimo cha zao la pamba wilayani Bunda, warsha ambayo imeshirikisha
wadau mbalimbali wakiwemo, watendaji wa kata, maafisa ugani, maendeleo ya
jamii, ushirika, maafisa tarafa na waandishi wa habari.
Mirumbe amesema kuwa
zaidi ya shilingi milioni 464. 2 zinadaiwa kutoka kwa wakulima wa zao la pamba
waliokopa pembejeo ikiwemo mbegu pamoja na madawa ya kunyunyuzia zao hilo,
kutoka kwa makampuni hayo ambayo yalikuwa yanasambaza pembejeo hiyo.
Amesema kuwa wakulima
hao walikopa pembejeo hiyo kwa makubaliano kwamba watakapouza pamba yao
watalipa madeni hayo, lakini hadi sasa hawajal;ipa kiasi hicho cha fedha na
kwamba ifikapo septemba 30 mwaka huu, mkulima ambaye atalipa dfeni lake
atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kwa mjibu wa taarifa
iliyotolewa kwenye warsha hiyo, kampuni ya S&C Ginning Co. Ltd, inadai
kiasi cha sh. 177,169,400, Allience Ginneries Ltd sh. 62,346,990, Olam Tanzania
Ltd sh. 98,105,880, Badugu Ginning Co. Ltd 108,789,000 na Mohamed (MeTI)
13,790,500.
Kufuatia hali hiyo
mkuu wa wilaya ya Bunda, amewaagiza watendaji wa vijiji na kata, pamoja na
maafisa ugani kufuatilia wakulima hao ili waweze kulipa madeni yao kwa
makampuni hayo haraka iwezekanavyo na kwamba kwani msimu wa kilimo kartibu
unaanza na wakulima hao watahitaji tena pembejeo hiyo, ambayo itasambazwa na
makampuni hayo.
Wakati huo huo Bw.
Mirumbe amewaagiza maafisa ugani kutembelea wakulima mashambani na sio kukaa
ofisini kama walivyozoea kwani kazi yao kubwa ni kutembelea wakulima na
kuwapatia elimu juu ya kilimo chenye tija.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment