Home » » MADIWANI BUNDA WATAKA MAKABRASHA YA VIKAO YAANDIKWE KWA KISWAHILI, WASEMA HAWAJUI KIINGEREZA

MADIWANI BUNDA WATAKA MAKABRASHA YA VIKAO YAANDIKWE KWA KISWAHILI, WASEMA HAWAJUI KIINGEREZA

Mwandishi wetu, Bunda-Mara Yetu
MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Bunda, mkoani Mara, wameagiza idara zote katika halmashauri hiyo, kuandika makaburasha kwa ajili ya vikao vyao kwa lugha ya Kiswahili, badala ya kuandikwa kwa luga ya kiingireza kwa kile walichosema kuwa madiwani wengine hawaijuhi lugha hiyo.
Madiwani hao walifikia hatua hiyo jana kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Bunda, baada ya kukuta kaburasha la taarifa ya ofisi ya mipango limeandikwa kwa lugha ya kiingireza.
Kufuatia taarifa hiyo kuandikwa kwa lugha ya kiingereza madiwani hao walikataa kuipitisha taarifa hiyo na kusema kuwa kuanzia sasa wanatoa agizo kwa halmashauri hiyo kuhakikisha makaburasha ya vikao vyao yanaandikwa kwa Kiswahili, ili wawe na uwezo wa kuhoji vizuri.
Aidha, walimtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Bw. Cyprian Oyier, kusimamia suala hilo hili lisijitokeze tena kwa kile walichosema kwamba walikwishapitisha azimio hilo lakini bado halijatekelezwa.
Wamesema kuwa katika kikao kingine kijacho taarifa hiyo ya idara ya mipango iletwe ikiwa imeandikwa kwa Kiswahili na kuchanganua mambo yote ya mipango ikiwa ni pamoja na miradi inayotekelezwa na kiasi cha fedha kilichotengwa kwa miradi husika.
Aidha, katika kikao hicho, kilichokuwa chini ya mwenyekiti wa halmashauri hiyo, mheshimiwa Joseph Malimbe, madiwani hao walimchagua tena Bw. Sospeter Masambu, kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo, ambapo pia waliunda kamati za halmashauri hiyo.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa