Mkazi mmoja wa Kijiji cha Kwisarara katika
Kata ya Bumera, wilyani Tarime, ameuawa kwa kukatwa mapanga wakati wakiwa
kwenye sherehe ya arusi nyumbani kwa mkazi mwingine wa kijiji hicho.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bumera, Sospiter
Marumi alimtaja aliyeuawa kuwa ni Mwita Kawawa (25).
Alisema mauaji hayo yamefanywa na mkazi mmoja wa
Kijiji cha Kitenga.
Alisema chanzo cha mauaji ni kupishana
lugha kati ya watu hao wawili wakati wakicheza disko.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Maalumu
wa Kipolisi Tarime/Rorya, Sweetbert Njewike, alithibitisha kutokea kwa mauaji
hayo ya Oktoba 26 mwaka huu.
Njewike alisema ugomvi kati ya watu hao, ulikuja
baada ya mtuhumiwa kumzuia Kawawa kuingia kwenye disko.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, mtuhumiwa huyo
ameshakamatwa na kwamba atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yake.
Aliwataka wananchi mkoani Mara, kuepuka
kujichukulia sheria mikonono na kuathiri maisha ya watu wengine.
Kamanda Njewike alisema mara mara kwa mara
wananchi mkoani humo wamekuwa wakijichukulia sheria mikononi kwa kuwaua wengine
wasiokuwa na hatia.
Alisema polisi hawatasita kuchukua hatua dhidi
ya watu wa aina hiyo, ili kukomesha vitendo visivyokubalika katika jamiii.
CHANZO MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment