Home » » SERENGETI WALIMU WADAI WAPEWE MADAI YAO

SERENGETI WALIMU WADAI WAPEWE MADAI YAO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

CHAMA cha walimu Tanzania (CWT)  wilaya ya Serengeti  mkoani mara
kimeunga mkono tamko  la CWT  taifa la kuwataka  walimu wa shule za
msingi na sekondari kugoma mwishoni mwa  mwezi huu  ili  kushinikiza
serikali kulipa mdai yao.
Katibu wa CWT wilaya ya Serengeti mbele ya wajumbewa mkutano mkuu wa
wilaya John Magoko amesema , walimu 335  wa shule ya msingi wanadai
sh.438,166,042  na walimu wa shule za sekondari 151  wanadai
shilingi163,477,725 baada ya uhakiki wa madai hayo ulio fanyika oktoba
2013
Amesema  kuwa  walimu  wastaafu zaidi ya kumi wameshindwa kusafirisha
mizigo yao kutokana na serikali kutowalipa kiasi cha sh,mil.9,hali
ambayo inazidi kuwaweka kwenye mazingira magumu na kwuadhalilisha.
Kwa upande wao wajumbe wa mkutano huo ambao ni walimu wamesema,mgomo
wao utahusisha kutoingia madarasani,ili kuishinikiza serikali kuwalipa
,kwa kuwa inawajali zaidi wanasiasa na kuwatelekeza wao,kwa kuwa madai
yao ni ya msingi na yamechukua muda mrefu bila kulipwa.
Madai hayo ni ya  fedha za uhamisho ,likizo, masomo, matibabu,
malimbiko  ya mshahara , kujikimu,  na fedha za walimu wapya na fedha
za mizigo ya wastafu
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa