Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKULIMA wa zao la
Kahawa Wilayani Tarime ambao wako kwenye vyama vya msingi vya ushirika wamesema
kuwa kupitia vyama hivyo
wamekuwa wakinufaika kwa kupata mikopo kutoka Benki ya NMB Tawi la Tarime na
hivyo kuwawezesha kuendelea na shughuli za kilimo kwakuwa upatiwa mikopo ya
fedha ambazo huwasaidia kutekeleza mahitaji
yakiwamo ya kilimo cha zao la kahawa.
Mwenyekiti wa Kamati ya wadau wa kahawa Kanda ya Mara
inayojumuisha Mikoa ya Mara,Mwanza na
Geita, Lucas Maasa ambaye ni mkulima wakahawa kikijiji cha Bungurere kata ya
Muriba alisema kuwa kupitia vyama vya
msingi Benk ya NMB imekuwa ikiwakopesha wakulima wakahawa fedha ambayo dhamana
yao ni kahawa wakati huo wakulima wakingoja mazao
yao kuuzwa.
Loice Mwita mkulima wa
kahawa kijiji cha Nyantira kata ya Nyansincha alisema kuwa mikopo ya fedha
wanayopata kutoka Benk ya NMB imewanufaisha,na kupitia vyama vya msingi huuza
kahawa kwa bei ya 1000 kwa kilo ambapo wakulima ambao hawajajiunga na vyama vya
msingi huuza kahawa yao kwenye makampuni binafsi kwa 600 kwa kilo ambayo ni
hasara kwa mkulima.
Hata hivyo Menieja wa
Benk ya NMB Tawi la Tarime Daniel Mubusi alisema kuwa lengo la kuwapatia mikopo
wakulima wa kahawa ni kuhakikisha nao wanajikomboa kimaisha kupitia kilimo cha
kahawa kwani nia ya NMB si kuwakopesha watumishi, wafanyabiashara na
wafanyakazi tu bali hata wakulima kwakuwa mazao yao ni dhamana kwao kuweza
kupatiwamikopo ambapo Benk hiyo ilizana kutoa mikopo kwa wakulima wakahawa
Tangu mwaka .
0 comments:
Post a Comment