Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WATU wawili wamekufa katika matukio tofauti wilayani Bunda, mkoani
Mara, akiwemo mwanamke mmoja aliyeuawa na mchumba wake na kufukia mwili wake
polini na kisha fisi kufukua kaburi hilo na kichwa chake kuonekana mitaani
kikiliwa na mbwa.
Tukio hilo la kikatili lililothibitishwa na polisi, limetokea
Aprili 22 mwaka huu, majira ya saa 3:00 asubuhi katika kijiji cha kiroreli
wilayani Bunda.
Mwanamke aliyeuawa na mchumba wake ametambuliwa kwa jina la
Wambura Magonze, mkazi wa kijiji cha Kiroreli.
Polisi wamesema kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hilo
walikwenda katika eneo la tukio wakiongozana na mkuu wa upelelezi wilayani
hapa, Munguwajuna, na kukuta mbwa mitaani wakila kichwa cha marehemu huyo.
Imeelezwa kuwa mwaume huyo baada ya kumuua mchumba wake kwa
kipigo, wakiwa wanatoka shambani aliuzika mwili wake polini katika kaburi lenye
urefu wa futi moja.
Aidha, imeelezwa kuwa baadaye wanyama wanaodhaniwa kuwa ni fisi
waliufukuwa mwili huo na kuanza kuula, na kwamba kichwa cha marehemu
kilionekana mitaani kikiliwa na mbwa.
Mwanaume huyo Matoka Maroba Isumail (24) mkazi wa kijiji hicho,
baada ya tukio hilo alitoroka, lakini baadaye akakamatwa na polisi na amekiri
kufanya mauwaji hayo.
Polisi wamesema kuwa awali mwanaume huyo aliandika ujumbe kwenye
vipande vya karatasi vipatavyo saba na kuvipeleka nyumbani kwa baba wa mwanamke
huyo, ambavyo vilikuwa na vitisho kadhaa.
Katika maelezo yake aliyotoa polisi mwanaume huyo amesema kuwa
aliamua kumuua mchumba wake huyo kwa sababu baba yake alikuwa anataka kumuoza
kwa mume mwingine kwa mahali nyingi, licha ya yeye kukubaliana kutoa mahali ya
ng’ombe saba na laiki sita, pamoja na kutoa kishika uchumba cha sh. 70,000.
Ameongeza kuwa baada ya kumuua mchumba wake yeye pia alikuwa anao
mpango wa kujiua na kwamba tayari alikuwa amekwishaandika historia ya maisha
yake ambayo ingesomwa wakati wa mazishi yake.
Mtuhumiwa huyo jana (yaani leo jumatano) amefikishwa kwa mlinzi wa
amani na akakiri kufanya mauwaji hayo, ambapo leo (yaani kesho) asubuhi
atafikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bunda, kujibu tuhuma hiyo.
Na katika tukio jingine lililotokea usiku wa kuamkia jana
jumatano, mwendesha pikipiki mmoja Kitaboka Maringo Matutu Issa, mkazi wa mjini
Bunda, ameuawa na mtu au watu wasiofahamika kwa kupigwa na kitu kizito
kichwani, pamoja na kuchomwa shingoni na kitu chenye ncha kali.
Tukio hilo ambalo pia lilithibitishwa na polisi limetokea katika
mtaa wa Manyamanyama kata ya Nyasura mjini Bunda.
Afisa mtendaji wa kata ya Nyasura, John Yapanda, amesema kuwa
mwendesha pikipiki huyo aliuawa kikatili na watu hao ambao pia walimpora
pikipiki yake.
Kamanda wa polisi mkoani Mara, kamishina msaidizi mwandamizi wa
polisi, Ferdinand Mtui, jana hakupatikana kuzungumzia matukio hayo, kutokana na
pilikapilika za shughuli za msiba wa mkuu wa mkoa wa Mara, John
Gabriel Tupa, aliyefariki dunia ghafula juzi akiwa wilayani Tarime, alikokuwa
amekwenda kufunga mafunzo ya mgambo.
0 comments:
Post a Comment