Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BENKI ya Uwekezaji Tanzania (TIB) imekopesha matrekta matatu yenye
thamani ya sh milioni 83 kwa wanachama watatu wa Chama cha Kuweka na
Kukopa cha Chiringe kilichoko mjini Bunda, Mara ili walime kisasa na
kuinua uchumi.
Waliopata matrekta hayo ni Robert Masatu, Opigi Ocharo na Nyerere
Odera wote wakazi wa Bunda ambao watarejesha mkopo huo kwa miaka minne.
Mkopo huo ulikabidhiwa mjini hapa jana na Ofisa Ushirika wa wilaya
hiyo, Saulo Lunyeka na kusema umetolewa na benki hiyo ili walime kwa
ufanisi badala ya kilimo cha jembe la mkono.
Aliwaasa wanachama hao kurejesha mkopo huo kwa muda muafaka ili
wengine wakope, huku akiwataka wananchi kujiunga kwenye vikundi wapate
fursa ya kukopeshwa.
Mwenyekiti wa chama hicho, Robert Masatu, alisema walianza kuomba
mkopo huo mwaka 2012 na kwamba matrekta hayo yatawasaidia wakulima
wenye mashamba makubwa.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment