ZIARA ya waandishi wa habari wilayani Bunda, mkoani Mara, kupitia umoja wao kwa shule za sekondari kwa lengo la kujionea ujenzi wa maabara katika shule za kata, umefurahishwa na hatua zilizofikiwa.
Waandishi hao ambao walitembelea sekondari zote 24 za wilayani humo wameshuhudia ujenzi wa maabara ukiendelea ambapo sasa umefikia asilimia 73.
Waandishi wahabari hao ni Ahmed Makongo wa HabariLeo, Raphael Okello wa gazeti la Majira, Christopher Maregesi wa gazeti la Mwananchi, Sarah John wa Radio Mazingira FM na mpiga picha wa ITV Paschal Wagaka walitembelea sekondari hizo na kuelezwa na walimu kwamba ujenzi wa maabara hizo umefikia zaidi ya asilimia 73.
Baadhi ya walimu na wananchi walisema kuwa ujenzi huo umefikia hapo kwa sababu ya uhamasishaji na ufuatiliaji unaofanywa na mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe.
Mkuu wa wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe akihojiwa na waandishi hao ofisini kwake,baada ya ziara yao, alisema ujenzi wa maabara hizo unakwenda vizuri, licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo za kisiasa.
Mirumbe alisema wakati agizo hilo la Rais linatolewa, katika Wilaya ya Bunda kulikuwa na mabara saba tu kwenye shule hizo, lakini hadi sasa tayari wamekwishafanikiwa kujenga maabara 57.
Chanzo:Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment