Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia
Suluhu Hassan ukiwasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere ambako alika kusalimia familia hiyo na kuzuru kaburi la Baba wa
Taifa Mwalimu Nyerere, leo, katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama, akiwa
kaika ziara ya kufanya mikutano ya kampeni katika mkoa wa Mara.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan
akimsalimia mtoto wa sita wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere,
Madaraka Nyerere, alipowasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa
huyo, katika Kijiji cha Mwitongo, Bitiama mkoani Mara.
Mama Samia akisalimia wanafamilia wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere
Mama Samia akisalimia wanafamilia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
Chifu wa Ukoo wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, Japhet
Wanzagi, akimkaribisha na kutoa utambulisho kwa Mgombea Mweza wa Urais
Mama Samia Suluhu Hassan,
Aliyekuwa Muomba nia ya kugombea Ubunge jimbo la Nkenge, Asupta
Mshama, akipozi kwenye baadhi ya miamba ya mawe iliyopo katibu na kaburi
la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere, katika Kijiji cha Mwsenge,
Butiama mkoani Mara.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan
akiwasha mshumaa baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa
Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere, Mwitongo, Butiama mkoani Mara leo.
Mama Samia akishiriki kuomba dua kwenye kaburi la Baba wa Taifa,
Hayati Mwalimu Nyerere, kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara.
Mama Samia akiondoka baada ya kuzuru kaburi la Baba wa Taifa, Hayati
Mwalimu Nyerere. Butiama mkoani Mara. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
0 comments:
Post a Comment