Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa jimbo la Bunda
Mjini Esther Amos Bulaya amesema wanawake wana uwezo mkubwa wa kufanya
mabadiliko chanya katika jamii na kuliletea taifa maendeleo makubwa .
Bulaya ameyasema hayo
alipokuwa akizungumza na EATV kuhusu siku ya wanawake duniani leo ambapo
kauli mbiu inasema '50 kwa 50 2030: Tuongeze jitihada'.
''Malengo ya 50 kwa 50 kwa
wanawake inawezekana kwa wanawake wote tukiungana na kuwa kitu kimoja ,
si bungeni tuu bali tushikamane na kuonyesha kwa vitendo kwamba
tunawaweza kufanya kazi kwa kutumia fursa zilizopo nchini na kuondoa
dhana mbaya kwamba wanawake hatuwezi''.Amesema Bulaya.
''Mkoa wa Mara ni mkoa
mabao umeonyesha mfano kwa kupinga mila potofu za kuamini kwamba
wanawake hawawezi kwa kupata wabunge wa kuchaguliwa na wananchi ,mimi na
mwenzangu Esther Matiko wa Tarime mjini hii ni funzo kwamba wananchi
wanatuamini kwa kauli zetu na matendo yetu''-Amesisitiza Bulaya.
Aidha Bi Bulaya
amewakumbusha wanawake nchini kwamba wao ni jeshi kubwa na washikamane
katika kusimamia haki zao na kadri siku zinavyokwenda matukio ya
unyanyuasaji yatapungua katika jamii yetu.
Hata hivyo amebainisha kuwa
muamko wa elimu katika jamii hususani kwa watoto wa kike kuelimishwa
kumesaidia sana kupunguza vitendo vya mila potofu za ukeketaji,
kutomiliki ardhi pamoja na ukatili hasa katika mkoa wa Mara
ukilinganisha na miaka 10 iliyopita.
0 comments:
Post a Comment