Na Godfriend Mbuya
Mbunge
wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA Ester Bulaya amesema
wananchi wa jimbo lake watampika kutokana na namna anavyofanya kazi za
kuwatumikia kulingana na ahadi ambazo aliahidi.
Akizungumza
katika kipindi cha HOTMIX kinachorushwa na EATV, Bulaya amesema mara
baada ya kuchaguliwa na wananchi wa Bunda ameweza kusaidia mchakato wa
kutatua kero mbalimbali za wananchi kama ujenzi wa Zahanati, ujenzi wa
bweni, ujenzi wa madarasa, miradi ya maji, madawati mashuleni pamoja na
kugawa vifaa vya michezo kwa vijana ili waweze kushiriki michezo.
“Jimbo
langu lina changamoto kubwa sana za huduma za kijamiii, nimeanza
kukabiliana nazo kwa kuhakikisha kila senti tunayopata kwa ajili ya
maendeleo inatumika kama ilivyokusudiwa, na katika ubunge wangu mara
nyingi ninashinda jimboni ili kuhudumia wananchi kama nilivyoahidi”
Amesema Bulaya.
Aidha
ameongeza kuwa kati ya mambo aliyoahidi wananchi ni kuwa mtumishi na
siyo kuwa mtawala, hivyo kwa kufanya hivyo anaamini wanaqnchi watampima
kutokana na namna anavyotatua kero za wananchi.
Pamoja
na hayo ameongeza kuwa wananchi wengi walikuwa hawana uelewa juu ya
mfuko wa jimbo, ila yeye amefanikiwa kutumia mfuko wa jimbo kwa
kusaidiana na wajumbe wa mfuko huo katika kutatua kero za wananchi
katika maeneo mbalimbali ya jimbo lake.
“Pesa
za mfuko wa jimbo hutofautiana kutoka jimbo moja hadi jingine, hivyo
kwa upande wangu pesa ambazo nimepata nimeanza kuzitumia kukarabati
miradi mbalimbali na jambo hili linawajengea wananchi imani kubwa juu ya
matumizi ya fedha hizo na dhana ya ushirikishwaji wa mambo
yanayowahusu” Amesisitiza Bulaya.
0 comments:
Post a Comment