Imeandikwa na Samson Chacha, Tarime
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amefungua majengo mawili
ya ofi si ya usalama barabarani na la michezo huku akiwahimiza askari wa
jeshi hilo Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya kufanya kazi kwa weledi,
kuwa waadilifu, kujituma na kuwa na mahusiano na kushirikiana na
wananchi katika ulinzi wa taifa na kupambana na uhalifu.
Aidha, imefahamika kuwa madereva 12,280 wamekamatwa kati ya Januari
hadi Juni mwaka huu katika makosa mbalimbali ya usalama barabarani na
kutozwa faini ya Sh milioni 368.4. Akizungumza na askari hao wa Polisi
wa Tarime/ Rorya jana katika hafla ya uzinduzi wa majengo hayo
yaliyojengwa kwa gharama zaidi ya Sh milioni 40.
Kamanda wa Polisi wa Tarime/ Rorya, Henry Mwaibambe alisema majengo
hayo yamegharimu Sh 21,978,000, wakati jengo la michezo ambalo
halijakamilika linatarajiwa kukamilika kwa zaidi ya Sh milioni 25.
Alizitaja changamoto nyingine zinazokabili Kikosi cha Usalama Barabarani
ni gari, pikipiki za kufanya doria ili kudhibiti vitendo vya makosa ya
barabarani.
CHANZO HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment