Home » » WANAOKWEPESHA WALIPA KODI WAONYWA

WANAOKWEPESHA WALIPA KODI WAONYWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MKUU wa Wilaya Rorya mkoani Mara, Simon Chacha, amekemea baadhi ya watu wenye tabia ya kukwepesha walipa kodi.


Kauli hiyo aliitoa juzi kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikijadili na kupitisha taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

"Unapofika wakati wa kusimamia mapato kuna haja wataalamu pamoja na madiwani kuungana ili kuhakikisha mapato anakusanywa na asitokee yeyote kati yetu anatugeuka," alisema Chacha.

“Nimegundua kuna baadhi ya watu wasio itakia Rorya mafanikio badala yake watu hao wanatumia nafasi walionayo kutorosha baadhi ya walipa ushuru wa halmashauri katika masoko na minada na kuikosesha mapato.” Joseph Sasi, aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa Mara, aliliambia baraza hilo kuwa Halmashauri ya Rorya imepata hati safi baada ya kukaguliwa na CAG kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 katika maeneo ya miradi ya maendeleo, mfuko wa pamoja, (Basketi Fund),Tasaf, Mfuko wa Barabara, miradi ya maji pamoja na matumizi ya uendeshaji na kupata hati safi.

"Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za serikali katika taarifa yake alionyesha maeneo mbalimbali ya kufanyia kazi ya menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya Rorya kuwa ni pamoja na mapendekezo yaliyotolewa na CAG, taarifa zote za hesabu za halmashauri ziwe zinakuwa na viambatanisho ili kuondoa usumbufu wa kufuatilia," alisema.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Rorya, Charles Chacha, alisema halmashauri yake inadaiwa na wadau mbalimbali Sh. milioni 800 ambayo wanategemea kuilipa punde fedha zitakapo patikana.

Alisema halmashauri yake imepata hati safi kwa ushirikiano wa madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo na kuwaomba kuendelea kutoa ushirikiano kuhakikisha wanaendelea kupata hati safi miaka mingine inayokuja.

Diwani wa kata ya Nyathorogo (Chadema), Germay Lwande, alisema madiwani kwa ushirikiano na watumishi wataendelea kulinda hati safi.

"Tumapata hati safi kwa ushirikiano wa madiwani pamoja na watumishi na tutaendelea kulinda hati safi hiyo isiondoke," alisema Lwande.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa