Home » » TUTAKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MUSOMA -MAJALIWA

TUTAKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MUSOMA -MAJALIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inakamilisha ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara iliyoanza kujengwa mwaka 1980.

Atoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 15, 2018) wakati alipokagua ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kuwasili mkoani Mara kwa ajili ya ziara yake ya kikazi.Waziri Mkuu amesema Serikali itakamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa awamu, ambapo wataanza na eneo la mapokezi na vyumba vya madaktari.

Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya nchini, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuiamini na kushirikiana nayo.Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 ili ujenzi uendelee. Ujenzi huo ulianza mwaka 1980, ulisimama mwaka 1987 kuanza tena 2010.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudencia Kabaka baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma kuanza ziara mkoani humo Januari 15, 2017. Kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima,   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  majengo ya Shule ya  Secondari ya Ufundi Musoma akiwa  katika  ziara ya mkoa wa Mara Januari 15, 2017.Serikali imetoa shillingi bilioni 1.28 kwa ajilli ya ukarabati huo.  Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Samweli Kiboyi. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Mutta Venance. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitoka ndani ya bweni la Shaban Robert wakati  alipokagua ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma  akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara  Januari 15, 2017. Serikali imetoa zaidi ya shilling bilion 1.28 ili kugharimia ukarabati hou. 
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ya  Mwalimu Nyerere iliyopo Kwangwa mjini Musoma  akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 15, 2017. Kulia wake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa