Home » » MTOTO MCHANGA AOKOTWA HAI AKIWA AMETUPWA KWENYE MIBA.

MTOTO MCHANGA AOKOTWA HAI AKIWA AMETUPWA KWENYE MIBA.



Dinna Maningo, Tarime

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Marco Nega amewataka wanawake kuepukana na mimba zisizotarajiwa ili kuepukana na tatizo linaloendelea nchini la kutupwa kwa watoto wachanga pindi wanapozaliwa.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Nega alisema kuwa imefika wakati wanawake watambue umuhimu na haki ya mtoto ya kuishi kwani wanawake wamekuwa wakibeba ujauzito na kisha kutoa mimba huku wanawake wengine wakitupa watoto wachanga pindi wanapojifungua.

Nega alisema kuwa mnamo tarehe 10 siku ya jumapili asubuhi mtoto mchanga akiwa ameokotwa na msamalia mwema akiwa ametupwa kwenye fensi ya miba mtaa wa Bomani mjini Tarime alifikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu baada ya kuonekana mwili wake kuchomwa na miba.

"Wanawake wamepukane na mimba zisizotarajiwa hii itasaidia kupunguza tatizo la watoto wachanga kutupwa au kunyongwa pindi wazaliwapo,ikishindikana wafuate uzazi wa mpango hospitali inatoa huduma bure na siyo kutupa mtoto ambaye umemlea kwa miezi 9 tumboni leo hii mama anajifungua na kutupa mtoto huo ni ukatiki kwa mtoto asiye na hatia"alisema Nega na kuongeza:

"Tumempokea mtoto kutoka kwa msamalia mwema tunampatia matibabu kwa sababu alikuwa amechomwa na miba tumeitoa miba yote na kumpaka dawa na sasa anaendelea vizuri anapatiwa uduma ya kunyweshwa maziwa ya ng'ombe”
Alisema kuwa mama aliyemwokota ndiye aliyenae hospitalini akimlea wakati wakifanya maandalizi ya kumpeleka kituo cha Misheni cha kulelea watoto kilichopo Nyabange Musoma kwa kuwa Serikali haina vituo vya kutunza watoto kama hao wakifika hospitalini.
Hellena Bon alisema alimwokota mtoto huyo aliyekuwa ametupwa katika fensi ya miba Nyumbani kwakwe nakwamba yuko tayari kumlea mtoto huyo baada ya kutimiza miaka 2 atakayolelewa kwenye kituo cha misheni Musoma.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha alisibitisha kuokotwa kwa kichanga hicho na kwamba hadi sasa hakuna aliyekamatwa kutupa mtoto huyo ambapo pia amewataka wananchi kwa kushirikiana na polisi kumbaini muhusika wa tukio hilo la kutupa mtoto.
Chanzo: Mwana wa Afrika

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa