Home » » Uhaba wa madawati bado ni changamoto kwa shule za msingi na Musoma Vijijini

Uhaba wa madawati bado ni changamoto kwa shule za msingi na Musoma Vijijini

UHABA wa madawati katika shule za msingi na sekondari umeendelea kuumiza vichwa vya wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla nchini, ikiwemo Shule za Wilaya ya Musoma Vijijini.

Upungufu wa madawati katika shule za msingi umeendelea kudidimiza kiwango cha elimu nchini huku ukichangia kuongezeka kwa utoro kwa kusababisha wanafunzi wengine kukata tamaa ya kusoma na mazingira ya shule kwa ujumla ambayo si rafiki kwao.

Matokeo ya wanafunzi kukaa chini husababisha wanafunzi kuandika wakiwa wameinama na wengine hata kulala kifudi fudi na wengine kuchuchumaa na hivyo kushindwa kuandika vizuri na pia kuchoka mapema. Hali hii kupelekea matokeo mabaya nyakati za mitihani hasa ya kitaifa.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Etaro wakiwa darasani wakimfuatilia mwalimu. wanafunzi wengi katika shule hii wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati.Picha na Habari ni kwa hisani ya Mdau Joachim Mushi.
Wakiwa wanamsikiliza Mwalimu darasani na wengine wakiandika kwenye madaftari ya mazoazi.
Wanafunzi wa shule ya msingi Etaro wakiwa darasani.Shule hii ipo wilaya ya Musoma vijijini.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa