Home » » MAAJABU: MTOTO AZALIWA NA VICHWA VIWILI

MAAJABU: MTOTO AZALIWA NA VICHWA VIWILI

na Berensi Alikadi, Bunda
MKAZI wa Mtaa wa Chiringe, katika mamlaka ya mji mdogo wa Bunda, Sarah Abidenego amejifungua mtoto akiwa na vichwa viwili.
Akizungumza na Tanzania Daima jana katika wodi ya wazazi katika Hosptali ya DDH iliyoko mjini hapa, mwanamke huyo alisema alipokuwa mjamzito alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo na kwamba Julai 24 majira ya saa 3:45 alijifungua mtoto wa kike akiwa na vichwa viwili.
Akielezea suala hilo, muuguzi wa zamu katika wodi hiyo, Sophaleti Majanjala, alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 1.9 na kwamba baada ya kuzaliwa alikaa muda wa saa moja na kufariki dunia.
“Huyu mtoto baada ya kuzaliwa aliishi kwa muda mfupi kama saa moja hivi na baadaye alifariki dunia , tunasubiri baadaye tuwakabidhi maiti kwa ajili ya kwenda kuzika,” alisema muuguzi huyo.
Mwanamke huyo alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa ndiye aliyempa kiumbe hicho na pia ndiye aliyekichukua na kwamba ana matumaini atabeba mimba nyingine na atazaa mtoto aliye na viungo vilivyokamilika, kwani hiyo ilikuwa ni mimba yake ya kwanza.
Alifafanua kuwa wakati akiwa na ujauzito huo hakupata shida ya kuuguaugua mara kwa mara, lakini wakati wa kujifungua alishangaa kuona anajifungua mtoto akiwa na vichwa viwili.
Tukio hilo lilivuta hisia za watu wengi ambao walifika katika wodi hiyo kutaka kukiona kichanga hicho, lakini kwa bahati mbaya walikuta tayari kimeshafariki dunia, hivyo hawakuruhusiwa kukiona.
Chanzo: Tanzania Daima

1 comments:

Prezden said...

Picha yake mbona hakuna jamani!

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa