Rorya, Mara
SERIKALI imedaiwa kupuuza maelekezo na ushauri wa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabe za serikali ya kutaka kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria,maafisa kadhaa waandamizi wa halmashauri ya wilaya Rorya mkoani Mara kwa tuhuma za ufisadi badala yake imewahamishia vituo vipya vya kazi.
Maafisa hao ambao wamehamishia katika vituo vipya vya kazi na katika halmashauri za Kiteto,Rukwe,Karagwe,Kwimba na Mafia pamoja na makao makuu ya mkoa wa Morogoro ilipendekezwa na ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katika taarifa yake ya ukaguzi maalum ya machi 2011 kuwa maafisa hao wasimamishwe kazi na kufikishwa katika vyombo vya dola.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya CAG,maafisa walikuwa wa wilaya ya Rorya ambao walipaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa tuhuma za kusababisha ubadhilifu wa zaidi ya milioni 200 ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka vibaya ni aliyekuwa mkurugenzi,mweka hazina,afisa raslimali watu mwandamizi,mhandisi wa ujenzi wilaya,afisa mipango wilaya na afisa ugavi daraja la pili.
Kufuatia hatua hiyo ya serikali ya kuwapangia vituo vipya vya kazi watumishi hao licha ya CAG kubaini kuwa wana tuhuma za kujibu,baadhi ya madiwani wa CCM katika halmashauri ya Rorya,wametangaza kuwa endapo serikali itashindwa kuchukua hatua ndani miezi mitatu kuanzia sasa wako tayari kukiama chama chao katika kuwatendea haki wananchi.
Hata hivyo ripoti hiyo ya CAG imeipendekeza kwa baadhi ya watumishi kupewa adhabu ya kalipio kali,kuonywa na kukatwa mishahara yao kulingana na makosa waliyobainika kuyafanya.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo wtumishi wa kundi lilitakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria ni Bw Edwin Nyamsekela,Bw Chacha Moseti,Bw Alex Bw Albinus na Samwel Coyhuku CAG akipendekeza kesi ikianza itabidi watumishi hao wasimamishwe kazi mpaka kesi itakapomalizaka.
Hababari kwa hisani ya MWANA WA AFRIKA BLOG
0 comments:
Post a Comment