Dinna Maningo,Tarime
WATU watatu WAKAZI WA Kijiji cha magena kata yaTurwa Wilayani Tarime Mkoani Mara wamewauwa kwa kupigwa hadi kufa na wananchi wenye hasira kali kwa madai ya kuhusika na wizi wa ng’ombe .
Akiongea na Waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha alisema kuwa watu waliouwawa wanatuhumiwa na wananchi kwa kujihusisha na wizi wa mara kwa mara kijijini hapo ambapo wananchi walijichukulia sheria mkononi kuwauwa kwa madai ya kuiba ng’ombe.
Kamanda kamugisha alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 6 .30 usiku huko kalibu na Mto Nyamiobo katika kijiji cha Magena ambapo aliwataja waliouwawa kuwa ni Ndiege Nyamhanga {25} Mang’iti Kamunu{30} na Nyaikore Simion {42}.
Alisema kuwa watu hao waliuwawa kwa kushambuliwa kwa silaha za jadi na kisha kuwachoma moto nakwamba chanzo cha mauwaji hayo ni wananchi kuwatuhumu watu hao kuiba ng’ombe ambapo miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi kwa mazishi na kuwa juhudi za kuwasaka waliohusika na tukio hilo zinaendelea.
Kamugisha aliwaasa wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwa watu wanaowatilia mashaka na badala yake watoe taarifa katika vituo vya polisi ili sheria zichukuliwe dhidi yao
Kwa hisani ya Mwana Africa Blog
0 comments:
Post a Comment