Na Mwandishi Wetu, Musoma
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi wa Naibu Meya wa Manispaa ya Musoma kwa kura 13 dhidi ya nne.
Katika uchaguzi huo uliofanyika jana, mgombea wa CHADEMA, Bwire Bwire, ambaye ni Diwani wa Kata ya Mwisenge, alipata kura 13 dhidi ya kura nne alizopata mgombea wa CCM, Ali Hersy.
Mbali ya kupata nafasi ya naibu meya, pia wagombea wake, walifanikiwa kushinda uenyekiti wa kamati zote za manispaa hiyo, ambapo Diwani wa Makoko, Aloyce Mawazo, alichaguliwa kuongoza Kamati ya Afya.
Naye, Diwani wa Kata ya Bweri, Zedi Sondoki, alichaguliwa kuongoza Kamati ya Fedha na Uchumi, huku Diwani wa Kitaji, Siza Tarai, akichaguliwa kuongoza Kamati ya Mipango Miji.
Manispaa hiyo ina jumla ya madiwani 18, ambapo CHADEMA ina madiwani 11, CCM madiwani wanne na CUF madiwani watatu.
Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment