Home » » MTOTO AZALIWA BILA MIKONO NA MIGUU

MTOTO AZALIWA BILA MIKONO NA MIGUU

WAKATI Taasisi mbalimbali zikiendelea na juhudi kuelimisha wananchi kwaajili ya kipinga vitendo vya ukatili na mauaji ya kinyama wanayofanyiwa watu wenye ulemavu nchini,mtoto mmoja ambaye amezaliwa bila ya kuwa na mikono na miguu,yuko katika tishio la kuuawa baada ya baadhi jamii ya kijiji cha Muriaza kudai kuwa kuendelea kuishi kwa mtoto ni mkosi mkubwa katika kijiji hicho.

Mtoto huyo ambaye amezaliwa katika hospitali ya Butiama wilaya mpya ya Butiama mkoani Mara,anadaiwa kuwindwa na baadhi ya watu  kwaajili ya kumuua kwa imani potofu kuwa ni mkosi  katika  jamii  ya kabila  la  Wazanaki.

Mama  mazazi wa mtoto huyo Bi  Maria Joseph,mkazi wa kijiji  cha MURIAZA ambaye ni mwanafunzi kidato  cha  pili  katika  shule  ya  Sekondari  Bumangi,akizungumza katika hospitalini hapo alipohidhiwa ili kumlinda mtoto huyo,amesema licha wakazi wa kijiji hicho kutoa tishio pia wachimbaji wa madini wamekuwa wakimuwinda kwaajili ya kumdhuru kwa imani za kishirikina.

Kwa sababu hiyo ameomba jamii kumpa msaada kwani hivi sasa analazimika kuishi maisha ya kuomba omba kwani amedai hata mama ake mazazi amemugopo kutokana na kuzaa mtoto huyo wanamuita ni KITIMBA kwa jina la kizanaki.

Kwa  upande  wake moja ya Madaktari katika hospitali ya Butima Dk Getera Nyangi,amesema kitaalam tatizo hilo linasababishwa na matumizi ya dawa hasa za kienyeji ama vitu vya sumu vilivyotumiwa na mama akiwa mjamzito huku muuguzi  wa  zamu  katika  hospitali  hiyo Bi Yohana Joseph, akidai wamekuwa na kazi  kubwa ya  kumlinda  mama  na mtoto wake na matishio ya  mara kwa mara ya  watu wanadaiwa kutaka kumdhuru mtoto huyo.
Chanzo: Mwanawaafrika blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa