Home » » UKOSEFU WA SARE ZA MAKARANI WA SENSA WAKWAMISHA UTOAJI TAARIFA

UKOSEFU WA SARE ZA MAKARANI WA SENSA WAKWAMISHA UTOAJI TAARIFA



MUSOMA

WAKATI zoezi la Sensa ya Watu na Makazi likianza nchini kote,tatizo la ukosefu wa Sare maalum na Vitambulisho kwa Makarani ni miongoni mwa changamoto kubwa  ambazo zimejitokeza katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara na kusabisha baadhi ya wananchi kushindwa kutoa taarifa sahihi kwa makarani hao.
Baadhi ya makarani hao wa Manispaa ya Musoma,Butiama,Rorya na Serengeti kuwa baadhi ya kaya zimeshindwa kutoa taarifa sahihi kwa madai ya kutowaamini kwa vile tayari idara ya takwimu ya taifa ilitangaza katika vyombo vya habari kuwa kila karani atakuwa na sare maalum na kitambulisho cha kazi hiyo.

Mratibu wa Sensa wa mkoa wa Mara Bw Ramadhan Mbega,amekiri kupata taarifa hizo kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara jambo ambalo amesema limetokana na kuchelewa kwa vifaa hivyo kuwaomba viongozi wa mitaa,vitongoji na vijiji kuwatambulisha makarani hao kwa wananchi.

Katika hatua nyingine mkuu  wa mkoa wa Mara,Bw  John Tupa,amewataka wanancchi kujitokeza katika zoezi la Sensa na Makazi linaloendelea nchini kote huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Makarani ili kufanikisha Zoezi hilo.

Mkuu huyo wa mkoa wa Mara akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhesabiwa katika makazi yake,amesema zoezi hilo katika mkoa wa Mara limeanza vyema licha ya kuwepo kwa kasoro ndogo ambazo zinafanyiwa kazi.
Chanzo: Mwananwafrika blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa