Na Timothy Itembe, Tarime
MWANAFUNZI wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari Nyamwaga, Angelina Masero (17), ambaye ni mkazi wa Keisangura, ameuawa na mwanafunzi mwenzake wa kidato cha tatu kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime-Rorya, Justus Kamugisha, alisema tukio hilo lilitokea Julai 30, mwaka huu, saa tano shuleni hapo, ambapo mwanafunzi huyo alichomwa kisu sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kifo chake.
Alisema alichomwa kisu na Mhono Manko (22) anayedaiwa pia alikuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Alisema mwanafunzi huyo alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Wilaya Tarime Bomani kwa matibabu, wakati madaktari wakijitahidi kuokoa maisha yake.
Alisema baada ya mtuhumiwa kutenda kosa hilo alichukua uamuzi wa kunywa sumu inayosadikiwa kuwa ni dawa ya kuoshea mifugo kwa lengo la kutaka kujiua.
“Mtuhumiwa baada ya kutenda tukio hilo pia alijisalimisha Kituo cha Polisi Nyamwaga ambapo alipelekwa Kituo cha Afya Nyamwaga kwa matibabu, ameruhusiwa na yupo polisi kwa mahojiano na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili,’’ alisema Kamugisha.
Wakati huohuo, mkazi wa Kijiji cha Mika, wilayani Rorya, Sedeki Steveni (17) alitoweka nyumbani kwao kwa mazingira ya kutatanisha bila kuaga ambapo kesho yake asubuhi mwili wake uliokotwa ukiwa unaelea juu ya maji katika Ziwa Victoria.
Alisema mwili wa marehemu unafanyiwa uchunguzi na madaktari na hatimaye kuzikwa nyumbani kwao.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment