Na Benjamin Masese, Dar es Salaam
MZEE Theo Mnanka (70), anadaiwa kuuawa kwa kutolewa kafara katika mgodi unaomilikwa na Hellena Mniko wa Kijiji cha Sirori Simba, mkoani Mara kwa imani za kishirikina.
Mzee huyo ambaye ni maarufu kutokana na kuwa na ndevu na sura yake kufanana na aliyekuwa kiongozi wa kundi la Alqaeda, marehemu Osama Bin Laden, alikutwa amekufa katika mgodi huo.,
Habari kutoka kijijini hapo zinasema, marehemu alikutwa kwenye shimo la machimbo ya dhahabu linalomikiwa na Mniko huku akiwa amenyofolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili.
Mgodi huo ni miongoni mwa migodi midogo iliyopo Buhemba na Majimoto inayotokana na mkondo wa mgodi mkubwa wa dhahabu wa Nyamongo (North Mara Barrick).
Inadaiwa kuwa, wakati wa tukio hilo, shimo hilo lilikuwa limekodishwa kwa Thomas Wambura, na marehemu alikuwa ni mlinzi kabla ya kuuawa kinyama.
Kutokana na marehemu kutoonekana kwa muda mrefu wanakijiji waliamua kumsaka, kabla ya kukuta ameuawa siku ya sikukuu ya Idd.
Polisi wa Kituo cha Kiagata waliitwa na kuufanyia uchunguzi mwili huo ambapo walikuta umenyofolewa sehemu za siri, ndevu na visigino vya miguu yote.
Taarifa za kifamilia zilizolifikia MTANZANIA, zinasema mtuhumiwa ni mmoja wa wanafamilia.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Makile Nyangalesi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema hakuna ushahidi wa kutosha kumtia hatiani mwenye mgodi.
Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Absalom Mwakyoma hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, kwani simu yake iliita bila kupokelewa.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment