Home » » PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA MBIO ZA MWENGE NYUMBANI KWA MWALIMU NYERERE WILAYA YA BUTIAMA

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA MBIO ZA MWENGE NYUMBANI KWA MWALIMU NYERERE WILAYA YA BUTIAMA

 Baadhi ya askari wa jeshi la polisi mkoa wa Mara wakiwa nje ya lango la Nyumba ya Baba wa taifa hayati Mwl Julius Nyerere wakingojea Mwenge wa uhuru ukiwa umechukuliwa kwenda kuwasha Mwenge wa Mwingo hivi karibuni.
 Kiongozi w mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2012 kapt Honest Ernest Mwanossa akitamka manane Sisi tumekwisha uwasha Mwenge na kuuweka mlima Kilimanjaro,baada ya kuwasha Mwenge uliopo Mwitongo Nyumbani kwa Baba wa taifa hayati Mwl Julius K Nyerere.
 Mbunge wa Musoma vijijini Mh Nimrod Mkono,akiongoza wakimbiza mwenge wa uhuru wakati wa kuwasha Mwenge wa Mwitongo
 Kapt Honest Mwanossa,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2012 akishuka baada ya kutekeleza wajibu wake wa kuwasha Mwenge wa Mwitongo ambapo kila mwaka Mwenge wa Uhuru lazima upite katika eneo hilo na kuwasha Mwenge huo Nyumbani kwa Baba wa taifa Hayati Mwl Julius Nyerere kijijini Butiama
 Wakimbiza Mwenge kitaifa na baadhi ya makamanda wa jeshi la polisi wakishuka baada ya kuwasha mwenge wa Mwitongo
Wakimbiza mwenge wa uhuru kitaifa,wakiongozwa na mkimbiza mwenge kitaifa mwaka 2012 Kapt Honest Ernest Mwanossa wakiweka mshada ya maua katika kaburi la Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo kijijini Butiama mkoani Mara hivi karibuni,baada ya Mwenge wa uhuru kuzuru nyumbani kwa Mwasisi wa Mwenge huo na taifa la Tanzania.

Picha na Maelezo kwa hisani ya George Marato

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa