Dinna Maningo, Tarime.
MAMA mmoja akiwa na watoto wake saba pamoja na wananchi wengine wawili wakazi wa kijiji cha Turugeti Kata ya Bumera Wilayani Tarime Mkoani Mara wameandamana hadi ofisi ya Mkuu Waliya ya Tarime wakidai kubomolewa nyumba zao jana na mtu mmoja aitwae Manyengo Lautent baada ya kudai kuwa eneo wanaloishi watu hao si lao bali walivamia.
Wakieleza malalamiko yao mbele ya katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime Hernest Kabohola walisema kuwa mnamo agost 28 majira ya saa 6 mchana Manyengo Laurent mkazi wa mjini Tarime alifika kijijini hapo akiwa ameongozana na kundi la watu zaidi ya 30 na polisi wa Kituo cha Turugeti na kisha wakaanza kubomoa nyumba zao kwa kile walichodai kuwa watu hao wamevamia na kuishi kwenye eneo la Manyengo Laurent.
“ Jana majira ya saa 6 Manyengo alikuja na kundi la watu akachukuwa polisi wa Turugeti wamebomoa nyumba zetu wanasema tuhame eneo hili tumehamia wakati wa oparesheni vijiji leo hii naambiwa nihame niende wapi na mi ni mzee! Serikali itusaidie sheria itumike ipasavyo”alisema Gitera Marwa.
Mwita Mkori alisema kuwa anashangaa kuona nyumba yake inabomolewa kwani hajawahi kushitakiwa mahali popote kuhusu eneo hilo lakini nyumba yake imebomolewa bila taratibu za kisheria kufuatwa licha yakuwa eneo hilo alilimiliki tangu wakati wa oparesheni vijiji mwaka 1974.
Rhobi Ryoba alisema kuwa kitendo cha nyumba yake kubomolewa na kutakiwa kuachia eneo limeathiri familia yake kwakuwa hawana mahali pa kuishi yeye na familia yake ambapo kwa sasa wanaifadhiwa na majirani.
“Nitaenda wapi nawatoto 7 na nina ujauzito mme wangu yuko jela alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na mahakama ya Mwanzo Tarime kutokana na tatizo hilihili la Manyengo Laurent, Mahakama ikaamuru nyumba yangu ibomolewe kuwa eneo si letu leo wamekuja wamebomoa japo eneo hilo tumeishi tangu wakati wa oparesheni vijiji wakati huo manyengo akiishi Dar es Salaamu baadae akahamia mjini Tarime na sasa kaja kijijini anadai eneo ni la babu yake kashitaki mme wangu na kisha amebomoa Naomba msaanda wa Serikali utatue tatizo hili”alisema Rhobi
Katibu tawala wa Wilaya ya Tarime Hernest Kabohola aliwataka wananchi hao kurejea katika uongozi wa Serikali ya kijiji ili tatizo lao lishughulikiwe kwakuwa wao ndio wanatambua eneo kwa uhalisia.
Mtendaji wa kijiji cha Turugeti Matiko Chegere alisema kuwa wananchi hao ndio wamiliki halali wa eneo kwani wameishi kwa muda mlefu tangu wakati wa oparesheni vijiji na kuwa anasikitika wananchi wengine kubomolewa nyumba kwakuwa hawajawahi kushitakiwa mahali popote na wala ofisi yake na uongozi wa serikali ya kijiji haukupewa taarifa na Manyengo Laurent kuhusu ubomoaji wa nyumba,nakwamba eneo si la Manyengo Laurent.
Kamanda wa polisi Tarime/Rorya alipohojiwa kama ana taarifa juu ya polisi wake kuhusika katika zoezi la ubomoaji nyumba alisema ofisi yake haina taarifa hiyo na hivyo kuahidi kufatilia swala hilo kwa ukaribu.
Chanzo: Mwanawaafrika blog
0 comments:
Post a Comment