Home » » WANANCHI TARIME WATAKIWA KUWEKEZA KATIKA KILIMO.

WANANCHI TARIME WATAKIWA KUWEKEZA KATIKA KILIMO.

Mwandishi wetu, Tarime
WANANCHI Wilayani Tarime wametakiwa kujikita katika kilimo cha mazao mbalimbali  kutokana na Wilaya hiyo kuwa na misimu miwili ya kilimo jambo ambalo litawawezesha kuendesha maisha yao endapo watawekeza katika kilimo hicho.
Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Tarime Selvanus Gwiboha alisema kuwa Wilaya ya Tarime ina uhakika wa chakula kwa mwaka  na ardhi yenye rutuba ya kutosha ambapo katika msimu huu wa masika Wilaya inatarajia kuvuna  tani 180,106 na msimu wa vuli utaanza Septemba 2012 hadi Januari 2013.
Gwiboha alisema kuwa kwa Wilaya ya Tarime eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 790,630 ambapo eneo linalolimwa ni Hekta 69,155 sawa na asilimia 76.30 eneo linalofaa kwa kilimo.
Gwiiboha alisema kwa upande wa upokeaji na usambazaji wa vocha za pembe jeo Wilayani Tarime ilipokea jumla ya Vocha 18,000 za kutosheleza wakulima 18,000 sawa na ekari 18,000,mbolea tani 18,000,Urea tani 18,000 na mahindi chotara tani 18,000 nakwamba thamani ya vocha zote ni 1,296,000,000, pia jumla ya vijiji 89 vimenufaika na ruzuku za pembe jeo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa