Home » » DIWANI WA ZAMANI AUAWA

DIWANI WA ZAMANI AUAWA

na Igenga Mtatiro, Tarime
DIWANI wa zamani wa Kata ya Kibasuka, Godfrey Gisururi (50), ameuawa kwa kupigwa risasi na kisha kukatwakatwa kwa mapanga na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Hata hivyo, ilielezwa kuwa licha ya kufanya mauaji hayo, watu hao wajachukua kitu chochote. Gisuri aliuawa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake, majira ya saa 2 usiku katika kitongoji cha Mwara, Kijiji cha Nyarwana alipokuwa nje na familia yake.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Diwani wa Kibasuka, Selemani Moya, alisema diwani huyo wa zamani alikutwa na mauti baada ya kupigwa risasi kichwani na watu hao.
“Sasa hivi ninaelekea katani, nimeambiwa kwa simu na ndugu wa marehemu huyo habari za kuuawa kwake na nikifika nyumbani nitakwenda kwenye msiba nipate taarifa zaidi,” alisema Moya.
Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata ya Kibasuka, Simon Imory, alikiri kutokea kwa tukio hilo na taarifa zimefikishwa Jeshi la Polisi Tarime na Rorya.
Ndugu wa marehemu, Joseph Chegere, alisema ndugu yake huyo alivamia na watu waatu walipokuwa wameficha sura zao na kwamba baada ya tukio hilo walitoweka bila kuchukulia kitu chochote.
“Baada ya kufanya mauaji hayo, watu hao walimbandika karatasi kwenye mwili wake iliyoandikwa “mkumbuke walio ndani kwa sababu yenu na bado” alisema.
Gisururi alikuwa diwani wa kata hiyo katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2005.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa