Home » » 10,777 KUHITIMU MSINGI

10,777 KUHITIMU MSINGI

na Berensi Alikadi, Bunda
JUMLA ya wanafunzi 10,777 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka huu katika Wilaya ya Bunda, utakaofanyika kesho nchini kote.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Ofisa Elimu ya Msingi wa wilaya hiyo, Laban Bituro, alisema kati ya wanafunzi hao; wavulana ni 5,452 na wasichana ni 5,325.
Alisema wanafunzi hao wanatarajia kufanya mtihani huo katika shule 155 ambazo ni za serikali na shule 151 za watu binafsi na kwamba maandalizi yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa mtihani huo.
Bituro alisema wilaya hiyo imeandaa vituo 478 katika majimbo yote ya Mwibara na Bunda ambako mitihani hiyo itafanyika na kwamba maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100.
Alifafanua kuwa wilaya imejiandaa kuhakikisha mtihanai huo utafanyika kwa amani na utulivu na kwamba wasimamizi wote wamekula kiapo na kwamba yeyote atakayekiuka kiapo na kuvujisha mtihani atachukuliwa hatua kali.
“Tumewapa mafunzo ya kutosha na wamekula kiapo na kwa sababu ni walimu wana dhamana ya serikali nina imani kuwa wataifanya kazi hiyo vizuri,” alisema.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa