Home » » GARI LA SERIKALI LAUA MWANAFUNZI

GARI LA SERIKALI LAUA MWANAFUNZI

Na Dorothy Chagula, Musoma
MWANAFUNZI amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha gari la Serikali lenye namba za usajili STK 5830. Ajali hiyo, ilitokea jana saa moja asubuhi katika eneo la Mwisenge Madukani mjini Musoma Mkoani Mara.

Inaelezwa ilisababishwa baada ya dereva wa gari hilo, Emmanuel Isali, kuacha barabara na kuwagonga wanafunzi hao waliokuwa pembezoni mwa barabara wakitembea kwa miguu.

Gazeti hili, lilishuhudia gari hilo likipinduka pembezoni mwa barabara, baada ya kuwagonga wanafunzi hao waliokuwa wakielekea shuleni.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara, aliwataja majeruhi kuwa ni Andrea Pascal 15), aliyeumia shingo na mguu wa kulia na Jackson Masanga(15), ambaye amevunjika miguu, wote wakiwa ni wanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Makoko Day.

Alimtaja majeruhi mwingine kuwa ni Kibasa Joseph (20), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkendo, ambaye amejuruhiwa vibaya kichwani.

Dk. Alisema, alipokea majeruhi hao saa moja asubuhi na kuwapatia huduma zote za msingi.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa