Home » » TPB YATUMIA MIL. 20/- KUJENGA MADARASA

TPB YATUMIA MIL. 20/- KUJENGA MADARASA

na Sitta Tumma, Bunda
BENKI ya Posta Tanzania (TPB), imetumia zaidi ya sh milioni 20 kujenga vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Stephen Wassira iliyopo kitongoji cha Salakwa, wilayani Bunda, Mara.
Mkurugenzi wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, alisema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa vyumba hivyo na kusema vitasaidia wanafunzi kupata sehemu ya kusomea.
Alisema benki hiyo ilipokea maombi kutoka serikali ya Kijiji cha Maliwanda kuhusiana na uhaba wa madarasa na kwamba maombi hayo yalifanyiwa kazi kwa kutengewa sh milioni 15, lakini baadaye benki hiyo ililazimika kuongeza fedha ili kukamilisha vyumba hivyo.
“Benki ya Posta Tanzania imekuwa karibu sana kusaidia mahitaji ya jamii yetu. Mfano vyumba hivi vya madarasa benki imetumia zaidi ya sh milioni 20.
“Awali tulitenga sh milioni 15, lakini baadaye tukalazimika kuongeza hadi kufikia sh. milioni 20 kwa lengo la kukamilisha ujenzi huu,” alisema.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, aliupongeza uongozi wa benki hiyo kwa kuwekeza katika elimu shuleni hapo, na kwamba huo ni mfano mzuri wa kuigwa na taasisi, mashirika, makampuni na watu binafsi wenye uwezo.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa