Dinna Maningo, Tarime-Mara Yetu
KIKUNDI cha Tembo Mazingira kinachojishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara pamoja na uoteshaji wa miche kilichopo kijiji cha Nyabitocho kata ya Mbogi Wilayani Tarime Mkoani Mara kimesema kuwa kinategemea kupata mazao mengi baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kukipatia trecta yenye thamani ya milion 44,207,000 kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Wameyasema hayo wakati wakikabidhiwa trecta na Mkuu wa Wilaya ya Tarime John Henjewele ambaye alikuwa mgeni rasmi ,wanakikundi hao wamesema kuwa trecta hiyo itarahisisha shughuli zao za kilimo kwani itatumika kubeba mazao, mbolea na kulima ambapo kwa muda mlefu wamekuwa wakilima kwa kutumia majembe ya mkono (plau).
Afisa kilimo wa Wilaya ya Tarime Selvanus Gwiboha amesema kuwa kikundi cha Tembo kiliibua mradi wa trecta ambao uliingizwa kwenye bajeti mwaka 2010/2011 ambapo jumla ya 55,000,000 ilitengwa kwa shughuli hiyo na kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2011/12 trecta hilo limenunuliwa kwa thamani ya milioni 44,207,000 ikiwa na tela, jembe la kulimia na la harrow na kikundi kiliweza kuchangia asilimia 20% milioni 11,000,000 na kuweza kupata trecta kupitia mradi wa DADP.
Mkuu wa Wilaya John Henjewele aliyekuwa mgeni rasmi kwa kuwakabidhi trecta amewataka wanakikundi kuonyesha nidhamu umoja na mshikamano katika shughuli mbalimbali za kikundi ili wapate mapato mengi katika shughuli zao za kilimo.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment