Dinna Maningo, Tarime-Mara Yetu
WANANCHI wa Mtaa wa starehe mjini Tarime wameiomba Serikali kufukia korongo la starehe ambalo limekuwa kero kwao kwa muda mrefu nakwamba endapo lisipofukiwa huwenda kukatokea maafa makubwa hasa kwa kipindi hiki cha mvua ya erinino.
Wakiongea na VFM wamesema kuwa kutokana na kuwepo kwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa kuna hatari nyumba zilizopo kando kando mwa korongo zikabomoka baada ya korongo hilo kujaa maji.
Mwenyekiti wa Mtaa wa starehe Genkuru Tagaya (CCM) amesema kuwa kwa muda mrefu tangu mwaka 2005 korongo hilo limekuwa likipigiwa kelele na viongozi wa mtaa lakini hakuna hatua zozote za Seikali zilizochukuliwa ili kuwanusuru wananchi waishio pembezoni mwa korongo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Fidelis Lumato amesema kuwa korongo hilo ni kubwa sana na linahitaji kiasi kikubwa cha pesa ili kuboresha na hivyo Halmashauri haina pesa kwa sasa kwakuwa korongo hilo halikutengewa bajeti yake na hivyo kuwataka kuwa na subira katika kipindi kingine cha bajeti.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment