Na Raphael Okello, Bunda
SHIRIKA za Kuwasaidia Wazee nchini (SAWATA), mkoani Mara, limesema madiwani mkoani humo wameshindwa kushiriki maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani kwa sababu hawakutenga posho za kuwapa baada ya maadhimisho.
Malalamiko hayo yametolewa na wazee katika maadhimisho ya siku hiyo ambayo yalifanyika juzi mjini Bunda na kusisitiza kuwa, madiwani ni wawakilishi wa wananchi na makundi mengine ya
jamii hivyo hawapaswi kutanguliza masilahi binafsi.
“Kimsingi tunasikitika kwa kitendo cha madiwani wetu kushindwa kushiriki maadhimisho haya kwa sababu hakuna posho, shirika letu bado changa na wazee wanakabiliwa na kero nyingi.
“Tulitegemea madiwani wangesimamia sera za wazee katika halmashauri zao lakini leo wanatususia,” walisema.
Mkoa huo una halmashauri sita ambazo ni Rorya, Tarime, Serengeti, Bunda, Butiama na Manispaa ya Mji wa Musoma lakini hakuna diwani hata mmoja aliyeshiriki maadhimisho hayo.
Akizungumza kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ambaye alikuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo Bi. Karoline Wanzagi, aliwatetea madiwani wa Bunda na kudai walikuwa katika Kikao cha Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (FUM).
Akisoma risala ya wazee hao, Ofisa Mipango na Fedha wa SAWATA, Bw. Salvanus Duba, alisema changamoto ambazo zinawakabili ni pamoja na uelewa wa sera za wazee na tafsiri
potofu ya wazee kuwa ni wanaume pekee.
Aliongeza kuwa, tafsiri hiyo inachangia kupokwa kwa haki za wanawake wazee na kukandamizwa hasa katika maeneo ya vijijini kutokana na mila potofu.
Alisema sh. 50,000 wanayolipwa wazee wastaafu na Serikali kila mwezi si stahili zao pamoja na kulalamikia usumbufu wanaopata wanapofuatilia jijini Dar es Salaam mirathi ya watoto wao waliofariki hivyo waliiomba Serikali itoe malipo ya
miradhi kupitia hazina ndogo mikoani.
Walitaja kero zingine ni usumbufu wanaoupaata katika huduma ya tiba hospitalini na kwenye zahanati hivyo walipendekeza kliniki za wazee zifunguliwe haraka katika vituo vinavyotoa huduma za afya.
Katika risala ya Mkuu wa Mkoa huo, Bw. John Tupa, ambayo ilisomwa kwa niaba yake na Kaimu Katibu Tawala mkoani humo, Bw. Joseph Makinga, aliwaagiza Wakurugenzi wa halmashauri kufungua kliniki hizo na kuongeza kuwa, kero zingine za wazee zitatekelezwa baada ya kutungwa sheria.

Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment