Mwandishi wetu,
Bunda-Mara Yetu
MWALIMU mkuu wa shule
ya msingi Butakare, iliyoko wilayani Bunda, Bw. Ezekiel Janes Sariro, ameibuka
mshindi katika nafasi ya katibu wa uchumi na fedha wa chama cha mapinduzi (CCM)
wilayani Bunda.
Bw. Sariro ameibuka
mshindi baada ya kupata kura 114 na kuwashinda wapinzani wake, Bw. Athumani
Saranga (Mambo), aliyepata kura 19 na Bw. Kondoro Chanila aliyepata kura 13.
Aidha katika uchaguzi
huo ambao umefanyika jana, pia mfanyabiashara mmoja Bw. Mwikwabe Chinga,
ameshinda nafasi ya katibu wa uchumi na fedha, baada ya kupata kura 89 na
kuwashinda Bw. Sarat Mimi aliyepata kura 55.
Mgombea mwingine aliyeshindwa
katika nafasi hiyo ni Bw. Jonh Kitang’osa ambaye pia ni katibu wa mbunge wa
jimbo la Bunda, Stevin Wassira aliyepata kura 38 katika awamu ya kwanza na
kuondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Katibu wa CCM
wilayani Bunda, Bw. Nyigoti amesema kuwa katika uchaguzi huo pia wajumbe watano
watano wa halmashauri kuu ya CCM wilaya walichasguliwa.
Bw. Sospeter Nyigoti
amewataja wajumbe hao kuwa ni pamoja Bw. Paul Chikomati, B w. Mwita Mang’era,
Bi. Sophia Makamulo, Bw. Kanazi Frugence na Emmanuel Magoti.
Akihutubia katika
uchaguzi huo, mwenyekiti mteule wa CCM wilayani Bunda, Bw. Chacha Gimanwa,
amewataka wanachama wa chama hicho kuvunja makundi yao, bali wote waungane kwa
kukijenga chama hicho.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment