na Berensi Alikadi, Bunda
IDARA
ya Uvuvi wilayani Bunda, Mara imefanikiwa kukamata zana mbalimbali haramu za
uvuvi zipatazo 660 zenye thamani ya sh milioni 15.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Ofisa Uvuvi wa wilaya hiyo, Steven
Ochien’g, alisema zana hizo zilikamatwa kati ya Julai na Desemba mwaka jana.
Alisema
katika msako huo walioufanya katika vijiji vya Guta, Mwisenyi, Mayoro,
Nyamitwebili, Kibara, Kisorya na katika Kisiwa cha Nafuba walikamata zana
mbalimbali ambazo haziruhusiwi kuvua.
Alizitaja
zana zilizokamatwa kuwa ni makokoro ya sangara 45, makokoro ya dagaa 15, nyavu
za timba 20 na nyavu zenye matundu madogo 600 na kwamba mwaka huu wamefanikiwa
kukamata makokoro ya sangara 10 yenye thamani ya sh milioni 15.
Alibainisha
kuwa katika zoezi hilo watuhumiwa watano walikamatwa na kwamba kesi tatu zipo
mahakamani na nyingine upelelezi unaendelea.
Chanzo:
Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment