Home » » Mikutano Ya Ukusanyaji Maoni Ya Wananchi Tarime Leo Alhamisi

Mikutano Ya Ukusanyaji Maoni Ya Wananchi Tarime Leo Alhamisi



Wananchi wa kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadlliko ya Katiba leo alhamisi Nov. 22, 2012 katika kijiji hicho.

Mkazi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Bi. Grace Nyakola (33) akisoma nakala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha nyepesi wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Kata hiyo, leo alhamisi Nov. 22, 2012.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphery Polepole (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa wananchi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo leo alhamisi Nov.22, 2012. Wajumbe wengine wa Tume, wa kwanza kulia Nassor Mohammed, Maria Kashonda na Riziki Ngwali.

Wananchi wa Kata ya Mliiba Wilayani Tarime mkoani Mara wakisoma nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na machapisho mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo katika Kata hiyo, leo alhamisi Nov. 22, 2012


Na Ismail Ngayonga, Tarime, Mara

MKAZI wa Kata ya Kata ya Mliiba Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Marco Magubo (31) amependekeza ni vyema Katiba Mpya ikataze vyama vya siasa vinavyoingia madarakani mara baada ya kushinda uchaguzi wa Rais visipeperushe bendera yake na badala yake kuweka bendera ya Taifa.
Akitoa maoni yake leo (Alhamisi Nov. 22, 2012) kuhusu Katiba Mpya kwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alisema kitendo cha kupeperusha bendera ya chama kilichoingia madarakani kitaongeza chuki kwa wanachama wa Chama kingine cha siasa kilichoshindwa uchaguzi.

Aidha Magubo alisema Rais anayeingia madarakani anawakilisha maslahi ya wananchi wote na hivyo si busara kwa Chama kilichoshida uchaguzi kupeperusha bendera ya Chama chao kwani Kiongozi huyo haongozi wanachama wa chama chake pekee bali wananchi wote katika taifa.

“Tazama Marekani ambao hivi majuzi tu walifanya uchaguzi mkuu wa Rais, katika kampeni za vyama vyao hatukuweza kuona bendera ya Republican wala Democracy ambavyo vyote vilishiriki uchaguzi na badala yake tuliona wananchi wakipeperusha bendera ya Taifa lao na hatukuona bendera ya Republican wala Democracy” alisema 

Alisema kwa kuwa Tanzania ni nchi ya umoja, amani na mshikamano ni vyema  Katiba Mpya ikewe kipengele cha kukataza bendera za vyama vyao na badala ya wamwachie Kiongozi aliyopo madarakani kutetea hoja za wananchi wote.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa