MBUNGE wa
Musoma mjini Vicent Nyerere(Chadema) amemtaka mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP)Said
Mwema kuchukua hatua sasa kuhusu mauji mauji ya kikatili ambavyo yameibuka
katika Manispaa ya Musoma na wilaya ya Butiama.
Akizungumza tukio hilo amesema katika kipindi cha mwezi mmoja tu zaidi
ya watu kumi na saba wameuawa huku wengine wakichinjwa kicha waujia kuondoka na
vichwa na viungo vyao vingine vya miili yao.
Alisema
pamoja na hali hiyo ambayo imechangia hofu kubwa kwa wananchi lakini hakuna
jitihada zozote zinazochukuwa kwaajili ya kukabiliana na vitendo hivyo vya
kinyama.
Aidha mbunge
huyo alimtaka pia Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua kwa wenyeviti wa kamati za
ulinzi na usalama wa wilaya hizo ambao amedai baadhi yao wameshindwa kusimamia
majukumu yao na kubaki kuendesha siasa wakati wananchi wakizidi kuawa kinyama
na wengine kuachwa na vilema vya maisha.
“Ni tatizo
kubwa ndani ya mwezi mmoja tu watu kumi na saba wameuawa kinyama na wengine
kuchinjwa lakini mbali na vyombo vya dola kukaa kimya hata nyinyi waandishi
mmeshindwa kujulisha umma kuhusu ukatili huu”alisema Nyerere na kuongeza.
“Rais mtoe
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya(DC) hapo Musoma amekalia siasa
na kuacha majukumui ya serikali katika kulinda raia na mali zao hii ni hatari
kubwa”aliongeza.
Hata hivyo
wakati mbunge huyo akitoa kauli hiyo,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
wa wilaya ya Butiama Angelina Mabula,ameliagiza jeshi la polisi kufanya kazi
usiku na mchana katika kuhakikisha linawatia mbaloni watu wote ambao wanahusika
na mauji ya kikatili ya raia.
Mabula
ambaye ni mkuu wa wilaya ya Butiama,alitoa agizo hilo juzi jioni baada ya
kuokotwa kwa mama mmoja Sabina Mkereri (46)ambaye alichinjwa na wauji kuondoka
na kichwa chake katika kijiji cha Kabegi kata kata ya Nyakatende.
“Nawaomba
wananchi mtoe ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha wahusika wote wanasakwa na
kuanzia sasa naagiza kuanza kwa vikundi vya ulinzi shirikishi kwaajili ya
kufanya kazi ya kuwasaka watu hawa usiku na mchana…jamani tunaipeleka wapi
Tanzania yetu yenye amani kwa kufanya matendo haya ya kinyama”alisema DC
Mabula.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Butima Yohana Mirumbe na mwenyekiti wa
halmashauri ya Musoma vijijini Magina Magesa,walisema ni wajibu wa polisi
kuhakikisha inapambana na unyama huo unaendelea katika wilaya hizo hatua ambayo
imejenga hofu kubwa kwa wananchi.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Mara SSP Japhet Lusingu,amekiri kutokea kwa matukio
hayo huku akisema jeshi la polisi limejipanga kikamilifu katika kukabiliana na
mauji hayo ambayo yameibuka katika siku za hivi karibuni.
Wakati huo
huo kaimu kamanda wa polisi mkoani Mara, SSP Japhet Lusingu,amethibitisha
kutokea kwa kifo cha Eustace Nyarugenda ambapo amesema tukio hilo limetokea usiku wa Desemba
nne katika nyumba ya wageni ya Savana Bar and Guest house mjini Bunda.
Amesema wahudumu
wa nyumba hiyo walisikia mtu huyo ambaye ni mwanaharakati wa ABC Foundation la kutetea haki za wanawake na
watoto walisikia akikoroma na baada ya kutoa taarifa polisi walivunja mlango na
kukuta akiwa katika hali mbaya na baada ya kufikishwa hospitali ya DDH
alifariki dunia muda mfupi wakati akipatiwa matibabu.
0 comments:
Post a Comment