Mwandishi wetu, Mara Yetu
MKUU wa Mkoa wa Mara John Tuppa amewaagiza Watendaji wa Vijiji na kata katika kata ya Mwema na Nyamaraga Wilayani Tarime kufyeka mashamba ya mazao yote yaliyodaiwa kulimwa katika maeneo ambayo yalizuiliwa na kuchukuliwa na Serikali na kwamba kuendelea kulima katika maeneo hayo ni viashiria vya mapigano kati ya jamii ya Wakurya wa koo ya Wakira na Wanchari ambapo eneo hilo limekabidhiwa kwa jeshi la JKT.
Hayo ameyaeleza wakati wa ziara yake katika viwanja vya kijiji cha Nge'reng'ere kata ya Nyamaraga eneo kulikokuwa na mgogoro wa ardhi na mipaka ambapo ilielezwa kuwa kuna watu wa kijiji cha Kubiterere, Korotambe kata ya Mwema na kijiji cha ng'ereng'ere kata ya Nyamaraga wamekuwa wakilima mazao katika maeneo yaliyozuiliwa na Serikali jambo linalodaiwa kusababisha ugomvi.
RC Tuppa amemtaka Mkuu wa Wilaya Tarime John Henjewele kukutana na wazee wa mila kwa mazungumzo ikiwa ni pamoja na kuhakiki upya mipaka ya kijiji na kijiji ambayo imedaiwa kuwa ndiyo chanzo cha migogoro inayosababisha ugomvi inayopelekea watu kuuwawa na ujeruhiwa na mazao kuharibiwa.
Kwa upande mwingine RC Tuppa amewataka viongozi wa Tarime kutatua mapema matatizo ya wananchi nakwamba dharura inapotokea wanapaswa kukaa katika vikao vya kamati ya ulinzi na usalama ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo na sio kungoja tatizo linakuwa kubwa.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment