Home » » Wavuvi haramu Bunda wapewa wiki mbili kusalimisha za zao haramu

Wavuvi haramu Bunda wapewa wiki mbili kusalimisha za zao haramu



 
Mwandishi wetu, Mara Yetu
 
KUTOKANA na uvuvi haramu kushamiri katika Tarafa ya Kenkombyo, wilayani Bunda, mkoani Mara, Kaimu Ofisa Tarafa wa Tarafa hiyo, ametoa muda wiki mbili kwa wavuvi hao kusalimisha zana zao, vinginevyo watakaokamatwa baada ya muda huo watafikishwa mahakamani.
 
Kaimu Ofisa Tarafa ya Kenkombyo, Bw. Peter Abiud Jandwa, ameiambia Radio Free Africa, kuwa kwa sasa uvuvi huo, wa kutumia zana haramu, ambazo ni Timba, Makokolo pamoja na nyavu nyingine ambazo zina matundu madogo, umeshamiri sana katika tarafa hiyo.
 
Bw. Jandwa amesema kuwa kufuatia hali hiyo ametoa muda wa wiki mbili kwa wavuvi hao kusalimisha zana zao kwenye ofisi za vijiji, kata au Tarafa na hata kwenye viongozi wa vijiji na vitongoji, pamoja na viongozi wa BMU na kwamba watakaosalimisha ndani ya muda huo hawatachukuliwa hatua za kisheria.
 
Aidha, amebainisha kuwa hadi sasa baadhi ya wavuvi wamesalimisha zana zao, ambapo timba 12 za wavuvi kutoka katika kijiji cha Namibu, zimesalimishwa na kwamba pia makokolo matatu kutoka kwa wavuvi wa kijiji cha Mahyoro PIA yamesalimishwa.
 
Kusalimishwa kwa zana hizo kunatokana na agizo la la mkuu wa wilaya ya Bunda, Bw. Joshua Mirumbe, ambaye amekerwa na uvuvi huo ukiwemo uvuvi wa kutumia sumu, ambao umeibuka tena na akawataka viongozi wa maeneo yote yaliyoko kandokando ya ziwa Victoria kudhibiti hali hiyo.
 
Wakati huo huo, wananchi wanawatuhumu viongozi wa vijiji, kata na Tarafa, wakiwemo walinzi wa vikundi vya rasilimali katika ziwa Victoria (BMU), pamojanna polisi, kwamba wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya uvuvi haramu, na kwamba baadhi yzo wanapewa rushwa na kuruhusu uvuvi huo kuendelea.
 
Blogzamikoa
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa